Sport
Dollar
43,1870
0 %Euro
50,4976
0.25 %Gram Gold
6.424,1000
-0.1 %Quarter Gold
10.609,8100
0 %Silver
129,4000
-0.09 %Maandamano nchini Iran yameleta uharibifu mkubwa wa miundombinu ya nchi, baadhi ya ofisi za serikali, lakini hata nyumba za ibada zimeshambuliwa.
Vita vya maneno bado vinaendelea kati ya Marekani na Iran huku taifa hilo likikabiliana na maandamano makubwa yanayodaiwa kuchochewa na hali ngumu ya maisha.
Maandamano nchini humo yameleta uharibifu mkubwa wa miundombinu ya nchi, baadhi ya ofisi za serikali, lakini hata nyumba za ibada zimeshambuliwa.
Serikali ya Iran inasisitiza kwamba, maandamano hayo yamechochewa na Marekani na Israel na hata kuwakejeli waandamanaji kuwa, wanaharibu nchi yao, kumfurahisha Donald Trump Rais wa Marekani.
Mbali na msako mkali uliofanywa na serikali ya Iran na kamata kamata ya wanaodaiwa kuratibu maandamano. Kumekuwa pia na maandamano ya kuiunga mkono serikali lakini pia kuwapinga wanaoandamana dhidi ya uongozi wa nchi hiyo. Ilimradi kumekuwa na tafrani juu ya tafrani.
Kwa upande wake, Israel na Marekani wanayaangalia kwa karibu mno yanayojiri Iran, na kutaka kujua ni ipi hatma ya vurugu hizo.
Matarajio yao makubwa ni iwapo vurugu hizo zitakuwa na nguvu ya kuangusha utawala wa Kiislamu wa nchi hiyo ambao unadaiwa kuwa na tishio la uwezo wa nyuklia.
Katika moja ya hatua inayodhihirisha maandamano kuwa na ushawishi wa nchi za nje, ni pale waandamanaji wanapoomba msaada wa Trump, huku Trump nae akiitahadharisha Iran dhidi ya kutumia nguvu na kuahidi kutoa msaada kwa waandamanaji.
Yanayojiri nchini Iran yanaleta wasiwasi katika kanda, hasa ikizingatiwa umuhimu wa nchi hiyo na mataifa jirani, lakini pia kama mzalishaji mkubwa wa mafuta.
Mbali na hivyo, licha ya kutokuwa na uwezo wa kuishambulia Marekani moja kwa moja, Iran imesema, iwapo itashambuliwa na Marekani, basi nayo itashambulia kambi za Marekani zilizopo karibu na eneo hilo.
Mpaka sasa, ni vita vya maneno, ambapo kila mmoja anaonesha uwezo wake wa kubwatuka, huku kila mmoja akitafakari kwa makini hatua inayofuata.
Je, Trump atajiingiza katika mgogoro mwengine, kabla ya kumaliza ile aliyoianza?
Comments
No comments Yet
Comment