Sport
Dollar
43,1819
0 %Euro
50,3230
0.01 %Gram Gold
6.419,3800
-0.18 %Quarter Gold
10.609,8100
0 %Silver
128,5200
-0.77 %Marekani ilitangaza siku ya Jumatano kuwa inasitisha uchakatishaji wa viza za uhamiaji kutoka nchi 75, hatua ya hivi karibuni ya Rais Donald Trump dhidi ya wageni wanaotaka kuingia nchini humo.
Kwa muda mrefu Marekani imekuwa ikikataa kutoa viza kwa watu wanaoonekana kuwa huenda wakahitaji misaada ya serikali, lakini Wizara ya Mambo ya Nje ilisema sasa itatumia mamlaka hayo hayo kusitisha kwa jumla utoaji wa viza za uhamiaji kulingana na uraia wa waombaji viza.
“Serikali ya Trump inakomesha matumizi mabaya ya mfumo wa uhamiaji wa Marekani na wale wanaotaka kunufaika na utajiri wa wananchi wa Marekani,” alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Tommy Pigott.
Aliongeza kuwa, “Uchakatishaji wa viza za uhamiaji kutoka nchi hizi 75 utasitishwa wakati Wizara ya Mambo ya Nje ikifanya tathmini upya ya taratibu za uhamiaji ili kuzuia kuingia kwa raia wa kigeni wanaoweza kunufaika na misaada na huduma za umma.”
Misri miongoni mwa nchi zilizo kwenye orodha hiyo
Msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, aliandika kwenye mtandao wa X kwamba nchi zilizoathiriwa zitajumuisha Somalia, pamoja na Urusi na Iran.
Leavitt aliambatanisha kiungo cha makala ya Fox News iliyosema kuwa nchi nyingine zilizoathiriwa ni pamoja na baadhi ya mataifa yenye uhusiano mzuri na Marekani, yakiwemo Brazil, Misri na Thailand.
Wizara ya Mambo ya Nje haijatoa hadi sasa orodha kamili ya nchi zilizoathiriwa.
Trump hajaficha nia yake ya kupunguza uhamiaji wa watu wasiokuwa na asili ya Ulaya.
Zaidi ya watu 605,000 wamefukuzwa Marekani
Wizara ya Mambo ya Nje ilisema siku ya Jumatatu kwamba imefuta zaidi ya viza 100,000 tangu Trump aliporejea madarakani, idadi kubwa zaidi kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Wizara ya Mambo ya Ndani (DHS) ilisema mwezi uliopita kwamba serikali ya Trump imefukuza zaidi ya watu 605,000, na wengine milioni 2.5 waliondoka nchini humo kwa hiari yao wenyewe.
Hatua hii ya hivi karibuni haiathiri viza za watalii, biashara au aina nyingine za viza, zikiwemo zile za mashabiki wa soka wanaotaka kutembelea Marekani kwa ajili ya Kombe la Dunia la mwaka huu, ingawa serikali ya Trump imeahidi kuchunguza kwa kina historia za mitandao ya kijamii za waombaji wote wa viza.
Comments
No comments Yet
Comment