Sport
Dollar
43,1819
0 %Euro
50,3230
0.01 %Gram Gold
6.420,1900
-0.17 %Quarter Gold
10.609,8100
0 %Silver
128,6900
-0.64 %Maafisa wa kijeshi na wa kijasusi wa Israel wanasema maandalizi yanaongezeka kwa kasi kutokana na hofu kwamba Iran inaweza kulipiza kisasi katika maeneo mbalimbali endapo Marekani itaishambulia.
Israel imeongeza kiwango cha utayari wa kijeshi huku ikifuatilia kwa karibu kile ambacho maafisa na wachambuzi wanakielezea kama kuongezeka kwa uwezekano wa shambulio la Marekani dhidi ya Iran. Tathmini mjini Tel Aviv zimebadilika kutoka swali la kama Marekani itachukua hatua hadi lini itafanya hivyo.
Maafisa wa Israel wanaamini kuwa Marekani ingewaarifu mapema kabla ya shambulio lolote ili kuruhusu maandalizi dhidi ya uwezekano wa mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka Iran, yakiwemo mashambulizi dhidi ya ardhi ya Israel.
Kama tahadhari, Israel imeongeza viwango vya uangalizi na utayari katika vikosi vyake vyote vya kijeshi, hasa katika jeshi la anga na mifumo ya ulinzi wa anga.
Mwandishi wa masuala ya kijeshi Dorron Kadosh wa Redio ya Jeshi la Israel alisema kuwa maafisa wakuu sasa wanaona shambulio la Marekani kuwa haliepukiki.
“Tathmini ya Israel ni kwamba ikiwa Marekani itashambulia Iran, Kiongozi Mkuu Ali Khamenei ataamuru mashambulizi dhidi ya kambi za Marekani katika Mashariki ya Kati na dhidi ya Israel,” alisema.
Uratibu na Marekani umeongezeka
Wachambuzi wa Israel wanasema uratibu na Kamandi Kuu ya Kijeshi ya Marekani (US Central Command) umeimarika, huku ufuatiliaji wa kijasusi wa Irana na washirika wake wa kikanda ukiendelea.
Iran inaweza kulipiza kisasi kupitia kundi la Hezbollah nchini Lebanon, Wahouthi nchini Yemen, au mashambulizi kutoka Syria na Iraq, pamoja na operesheni za mtandaoni (cyber) na mashambulizi dhidi ya maslahi ya nje ya nchi.
Hata hivyo, maafisa wa Israel wanaonya kuwa Washington bado haijakamilisha mipango yake.
Wachambuzi wanaeleza kuwa chaguo za Marekani zinaanzia operesheni za mtandaoni na mashambulizi madogo ya kiishara hadi hatua kubwa za kijeshi ambazo zingehitaji kupelekwa kwa vikosi vikubwa, ikiwemo manowari za kubeba ndege za kivita na mabomu ya masafa marefu.
Ongezeko hili la tahadhari linakuja wakati Iran inazishutumu Marekani na Israel kwa kuunga mkono machafuko yaliyosababishwa na maandamano ya ndani, huku Rais Donald Trump akitishia waziwazi kuchukua hatua, akisema Washington ingewasaidia waandamanaji na kuionya Iran dhidi ya umwagaji damu zaidi.
Licha ya kuongezeka kwa mvutano, baadhi ya wataalamu wa usalama wa Israel wanahimiza tahadhari, wakisema hakuna dalili za uhakika za shambulio la karibu la Marekani au shambulio la haraka kutoka Iran, wakisisitiza hali tete na isiyotabirika ya mvutano huu.
Comments
No comments Yet
Comment