Sport
Dollar
40,8779
0.06 %Euro
47,6902
-0.1 %Gram Gold
4.379,2600
0.02 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Chama kikuu cha upinzani nchini Uganda kimewasilisha kesi katika mahakama ya katiba ili kufuta sheria mpya iliyorudisha haki ya mahakama za kijeshi kusikiliza kesi za raia.
Chama kikuu cha upinzani nchini Uganda Jumatano kiliwasilisha kesi katika mahakama ya kikatiba kupinga sheria mpya iliyopitishwa ambayo inarejesha haki ya mahakama za kijeshi kuwahukumu raia, wakili wa chama hicho alisema.
Mahakama ya Juu ilipiga marufuku kuwahukumu raia katika mahakama za kijeshi mwezi Januari 2025, ikisema haina uwezo wa kisheria wa kuendesha kesi za jinai kwa njia ya haki na isiyo na upendeleo.
George Musisi, wakili wa chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP), alisema chama hicho kimewasilisha ombi la kufuta sheria mpya ambayo bunge lilipitisha mwezi Mei na Rais Museveni kuisaini mwezi mmoja baadaye.
"Walikiuka taratibu zote ambazo walipaswa kufuata wakati wa kupitisha sheria," Katibu Mkuu wa NUP Lewis Rubongoya aliwaambia waandishi wa habari nje ya mahakama, akitaja ukosefu wa kushirikishwa kwa umma.
Jeshi laisifu sheria hiyo
Comments
No comments Yet
Comment