Sport
Dollar
40,8627
0.1 %Euro
47,7463
-0.26 %Gram Gold
4.374,9400
-0.56 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Wanaharakati wa Eswatini wameiomba mahakama kuu kuamua kuwa kinyume cha katiba hatua ya nchi hiyo kukubali kuwapokea raia watano wa kigeni ambao walifukuzwa Marekani.
Wanaharakati wa Eswatini wameitaka mahakama kuu kuamia kuwa ni kinyume cha katiba kwa nchi yao kukubali kuwapokea raia watano wa nje ambao walitimuliwa kutoka Marekani baada ya kuwepo gerezani kwa hatia ikiwemo mauaji.
Wanaume hao kutoka Vietnam, Laos, Yemen, Cuba na Jamaica walisafirishwa hadi katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika kwa ndege ya kijeshi ya Marekani mwezi Julai ikiwa ni sehemu ya mpango wa Marekani wa kuwapeleka wahamiaji katika mataifa ya tatu.
Katika shauri la dharura kwenye mahakama kuu ya Eswatini, mashirika matatu ya kisheria na ya kiraia yanasema makubaliano ni kinyume cha katiba kwa sababu hayakuwa yamewekwa wazi na hakukuwepo na mashauriano ya umma au bunge.
Walitaka serikali ya Eswatini kuweka wazi makubaliano kamili na Marekani.
Comments
No comments Yet
Comment