Umoja huo umelaani jitihada za kuingilia mambo ya ndani ya Somalia, ikisisitiza zinalenga kudumuza michakato ya upatikanaji amani, usalama na kujitawala kwa nchi hiyo.

Umoja wa Afrika wapinga Somalia kuingiliwa mambo yake ya ndani

Umoja wa Afrika (AU) umepinga na kulaani jitihada za kuingilia mambo ya ndani ya Somalia, kwa lengo la kuigawanya nchi hiyo.

Katika taarifa yake, umoja huo umelaani jitihada za kuingilia mambo ya ndani ya Somalia, ikisisitiza zinalenga kudumuza michakato ya upatikanaji amani, usalama na kujitawala kwa nchi hiyo.

AU ilisisitiza utayari wake wa kuendelea kuliunga mkono taifa hilo, katika azma yake ya upatikanaji amani na utulivu.

Katika hatua nyingine, Umoja wa Afrika uliunga mkono pendekezo la mpito kati ya AU na serikali ya shirikisho la Somalia, lenye kutilia mkazo wa kupunguzwa kwa walinda amani nchini Somalia, kuanzia Novemba 2026 hadi mwaka 2027.

TRT Afrika Swahili — TRT Afrika Swahili

Picha: Others

#