Sport
Mchakato huo wa mazungumzo uliongozwa na Rais wa Togo Faure Essozimna Gnassingbe.
Tume ya Umoja wa Afrika imefurahishwa na kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha makubaliano kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na M23.
Katika taarifa yake ya Alhamisi, AU imesema makubaliano hayo yanaashiria hatua muhimu katika kupunguza mapigano katika eneo la mashariki lenye mgogoro.
“DRC na kundi la M23 limesaini makubaliano Februari 2 mjini Doha kuhusu vipengele vya ufuatiliaji wa usitishwaji wa mapigano kufuatia mazungumzo ya Doha,” imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar wakati huo.
Qatar imeongeza kusema kuwa majadiliano yamefanyika ndani ya mpango wa Utaratibu wa Kusimamia Usitishaji Vita na Uthibitishaji.
Dhamira ya usitishaji vita
"Pande hizo mbili pia zimehuisha dhamira ya usitishaji wa mapigano na makubaliano ya Doha ya Amani yaliyosainiwa kati yao Novemba 15, 2025, na kuthibitisha dhamira yao na utekelezaji wa majukumu yote yaliyoainishwa kwa moyo mkunjufu, katika kuunga mkono mchakato wa amani," wizara imesema.
Mwenyekiti wa Tume ya AU Mahmoud Ali Youssouf amesema makubaliano hayo yanawakilisha “hatua ya ukuaji muhimu wa imani” na maendeleo chanya kuelekea kupunguza uhasama na kurudisha amani na utulivu mashariki mwa DRC.
Mchakato wa amani wa AU uliongozwa na Rais wa Togo Faure Essozimna Gnassingbe, ambae alichanguliwa na Umoja huo kuongoza mchakato wa majadiliano mashariki mwa DRC. Qatar na Marekani pia zilipongezwa kwa kuunga mkono jitihada za amani.
Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na wawakilishi kutoka Marekani na waangalizi kutoka Umoja wa Afrika, huku Togo ikishiriki katika nafasi yake kama mpatanishi kutoka AU.
Ufuatiliaji na uthibitishaji
Vikosi vya Ulinzi kutoka Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, na maafisa kutoka Mkutano wa Kimataifa wa eneo la Maziwa Makuu, pia wameshiriki, na kutoa msaada wa kitaalamu kuhusu ufuatiliaji wa usitishaji wa mapigano.
Tume ya Umoja wa Afrika imesisitiza kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa utaratibu unaoheshimika wa makubaliano ya usitishaji wa mapigano kutoka pande zote, ili kujenga imani kati ya pande zinazozozana.
Mashariki mwa Congo imekabiliwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi kadhaa ya waasi, ikiwemo M23.
Comments
No comments Yet
Comment