Sport
Dollar
38,7034
-0.18 %Euro
43,4811
0.23 %Gram Gold
3.995,3000
0.86 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Zelenskyy anatarajiwa kuongoza Ukraine, na ujumbe wa Urusi unatarajiwa kuongozwa na Vladimir Medinsky, msaidizi wa Putin mwenye ushawishi mkubwa na aliyekuwa waziri wa utamaduni ambae alihusika katika majadiliano ya 2022
Mahasimu wawili katika vita vya Ukraine na Urusi wanatarajiwa kuingia katika mazungumzo ya moja kwa moja kwa zaidi ya miaka mitatu, huku Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa hayupo katika orodha ya watakaohudhuria.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amemtaka Putin kukutana nae ana kwa ana jijini Istanbul Alhamisi, lakini ujumbe wa Urusi umetaka watu wa chini ndio watakaohudhuria mkutano huo.
Afisa mmoja wa Ukraine amesema hakukuwa na makubaliano ya lini mazungumzo na Urusi nchini Uturuki yataanza Alhamisi, na kupuuzia taarifa kutoka vyombo ya habari vya Urusi.Andriy Kovalenco, afisa kutoka Baraza la Usalama na Ulinzi wa Taifa, ameiambia Telegram kwamba kuanza kwa mazungumzo saa saa nne asubuhi (0700 GMT) “haikupangwa na sio kweli.”
Maelfu wameuawa tangu mapigano hayo yaanze mwezi Februari 2022. Urusi imekalia takriban sehemu kubwa ya eneo la Ukraine katika kile kinachojulikana kama mgogoro mbaya zaidi wa bara ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Putin alipendekeza kufanya mazungumzo Mei 15 jijini Istanbul baada ya Ukraine na mataifa mengine ya Ulaya kuitisha usitishaji wa mapigano wa siku 30 bila masharti.Zelenskyy alikubali, lakini alisema wiki hii kwamba iwapo Putin hatahudhuria yeye mwenyewe, itaonyesha kuwa hana dhamira ya kweli ya amani.
“Vita hivi…kwa hiyo, majadiliano yafanyike nay eye,” Zelenskyy amesema.
Ujumbe wa Kremlin utaongozwa na Vladimir Medinsky, msaidizi wa Putin na waziri wa zamani wa utamaduni ambae alishiriki mazungumzo ya mwaka 2022.
Putin, Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov na Yuri Ushakov, msaidizi wa sera za mambo ya nje wa Kremlin na Marekani hawakutajwa na Kremlin kuwa miongoni mwa wajumbe watakaoongoza mazungumzo hayo.
Comments
No comments Yet
Comment