Sport
Dollar
38,7897
-0.02 %Euro
43,4606
-0.04 %Gram Gold
3.961,8300
-2.26 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Trump amesema Mfalme Mohammed bin Salman na Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan wamemhimiza kukutana na Rais wa Syria al-Sharaa
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Marekani Donald Trump, Mohammed bin Salman kiongozi wa Saudi Arabia na Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa wamehudhuria mkutano kwa njia ya mtandao, Anadolu imeripoti Jumatano asubuhi.
Rais wa Uturuki Erdogan amesema uamuzi wa Rais wa Marekani kuondoa vikwazo kwa Syria una umuhimu wa kihistoria.
Trump, akiwa Riyadh katika ziara yake ya kwanza ya kiserikali tangu kuingia madarakani katika muhula wake wa pili, amekuwa rais wa kwanza wa Marekani katika kipindi cha miaka 25 kukutana na kiongozi wa Syria.
Viongozi hao wawili walifanya mazungumzo kwa muda mfupi kabla ya mkutano mkubwa wa viongozi wa Ghuba nchini Saudi Arabia wakati wa ziara ya Trump, amesema afisa wa ikulu ya White House.
Hakuna rais wa Marekani aliyekutana na kiongozi wa Syria tangu Bill Clinton kukutana na Hafez al Assad, baba wa Bashar, Geneva, mwaka 2000.
Trump alitangaza Jumanne kwamba anaondoa vikwazo “vya kikatili” vilivyowekwa katika utawala wa Assad kwa Syria kufuatia maombi ya washirika wa al-Sharaa Uturuki na Saudi Arabia-katika hatua yake ya hivi karibuni dhidi ya mshirika wake Israeli.
Israeli imepinga kuondolewa kwa vikwazo vya Syria, lakini Trump Jumanne amesema kwamba bin Salman na Erdogan wamemshajiisha kuchukua hatua.
Trump amesema ulikuwa ni “wakati wa Syria kung’ara” na kwamba kupunguza vikwazo “kutawapa fursa ya kuendelea.”
Wasyria wamefurahia habari hiyo, huku maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wakikusanyika katika uwanja wa Umayyad uliopo Damascus.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeuita uamuzi wa Trump “hatua muhimu” ambayo itasaidia kuleta utulivu.
Ziara ya Trump Mashariki ya Kati
Siku ya kwanza ya ziara ya siku nne ya Trump katika eneo la Ghuba ilikuwa ya sherehe kubwa na mikataba ya biashara, ikiwemo ahadi ya Saudi Arabia ya kuwekeza Marekani dola bilioni 600 na dola bilioni 142 katika ununuzi wa silaha za Marekani katika falme hiyo.
Baadae Jumatano, Trump atakwenda Doha, mji mkuu wa Qatar, ambapo atashiriki katika ziara ya kiserikali na Emir Sheikh Tamim bin Hamad al Thani na maafisa wengine.
Qatar, mshirika mkubwa wa Marekani, inatarajiwa kutangaza uwekezaji nchini Marekani wa mabilioni ya dola. Kufuatia ziara yake Qatar, Trump atakwenda Abu Dhabi kukutana na viongozi wa Umoja wa Falme ya Kiarabu.
Baada ya hapo atarudi Washington siku ya Ijumaa, lakini amesema anaweza kwenda Uturuki kwa ajili ya mazungumzo kati ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.
Comments
No comments Yet
Comment