Sport
Dollar
40,3631
0.13 %Euro
47,0418
0.38 %Gram Gold
4.353,7500
0.63 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Takwimu za Uganda Aida Commission zinaonyesha kuwa asilimia 70 ya maambukizi mapya ya ukimwi ni miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 ni hasa kwa miongoni mwa wasichana na wanawake vijana
Uganda imemua kuweke huduma ya kukumbana na Ukimwi katika huduma ya jumla ya Afya. hapoa awali ilikuwa chini ya huduma spesheli.
Peter Mudiope, Mratibu wa Kinga ya Ukimwi katika Wizara ya Afya, ametangaza kwamba Uganda inaunganisha huduma za kuzuia ukimwi na matibabu yake katika utoaji wa huduma za afya kwa ujumla kama sehemu ya jitihada za kuendeleza mwitikio wa kupunguza maambukizi mapya nchini humo huku rasilimali za nje zikipungua.
Akizungumza wakati wa mada kuhusu ushirikiano wa kukumbana na Ukimwi Mudiope alieleza kuwa Uganda inaoanisha mikakati yake na mbinu za kimataifa na kikanda sawa na zile zinazotekelezwa nchini Kenya, Rwanda, na Botswana ili kuhakikisha maendeleo endelevu katika kupambana na ukimwi.
Takwimu za nchi hiyo zinaonyehsa kuwa maambukizi mapya ya ukimwi yamepungua tangu mwaka 2010 kutoka 97,000 hadi takriban 37,000 kila mwaka.
"Miongoni mwa vijana wa kiume na wa kiume, ukosefu wa tohara pamoja na ngono zisizo salama husababisha asilimia 19 ya maambukizi mapya ya ukiwmi ,” alielezea Dkt. Vincent Bagambe, Mkurugenzi mtendaji Tume ya Ukimwi Uganda ( Uganda AIDS Commission)
"Asilimia 70 ya maambukizi mapya ya ukimwi ni miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 ni hasa kwa miongoni mwa wasichana na wanawake vijana."
‘Takwimu za Tume ya Ukimwi Uganda zinaonyesha kuwa watu 20,000 walikufa kutokana na hali zinazohusiana na Ukimwi licha ya kuwepo kwa matibabu ya kuokoa maisha na huduma za maabara.”- Dkt. Bagambe aliongezea.
Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa asilimia 94 ya watu wanaoishi na ukimwi wanajua hali yao huku asilimia 6 bado hawajapimwa.
90% ya wale wanaojua hali zao wanatumia madawa ya kukumbana na virusi vya ukimwi (ART).
97% ya wale wanaopata matibabu wamekandamiza virusi.
Zaidi ya watoto 70,669 chini ya miaka 14 wanaripotiwa wanaishi na virusi hivyo nchini Uganda kwa sasa.
Ni asili mia 80 tu ya watoto waliopimwa, 91% wako kwenye matibabu, na 89% wamekandamizwa na virusi hivyo.
Comments
No comments Yet
Comment