Dollar

40,3783

0.2 %

Euro

46,9885

0.37 %

Gram Gold

4.351,2500

0.57 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Edward Maingi Ndegwa alikutwa amekufa huku koo lake ikiwa limekatwa Julai, 17. 2025. Walioshuhudia walisema mwathiriwa alikuwa ni mlemavu.

Mshukuwa wa mauaji ya mgonjwa katika Hospital kuu Kenya akamatwa

Hospitali ya Taifa ya Kenyatta nchini Kenya imethibitisha kuwa mgonjwa mmoja aliuawa katika wodi katika mazingira yasiyoeleweka Julai 17 2025.

Kataika taarifa yake, Hospitali imesema itatoa taarifa zaidi pindi maelezo zaidi yatakapopatikana.

Maafisa wa upelelezi nchini Kenya wamesema walimkamata mshukiwa mkuu wa mauaji hayo ya kutisha yaliyotokea katika wodi ya Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH).

“Maafisa wa upelelezi wa mauaji wamemkamata Kennedy Kalombotole, mshukiwa mkuu wa mauaji ya kutisha ya wodi ya Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta,” DCI ilisema katika taarifa iliyoambatana na picha ya Kalombotole.

Kwa mujibu wa maofisa wa Idara ya Upelelezi wa Kitengo cha Makosa ya Jinai (DCI), kukamatwa huko kunafuatia mauaji ya kikatili ya Edward Maingi Ndegwa, mgonjwa aliyelazwa katika Wodi 7B, Kundi C , Julai 11, 2025.

Ndegwa alikutwa amekufa kitandani huku akiwa amekatwa koo Julai 17, 2025. Walioshuhudia walisema mwathiriwa alikuwa na ulemavu wa kimwili.

Kisa hicho kwa mara nyingine kimeleta hospitali ya KNH chini ya uangalizi, na kuibua wasiwasi mpya kuhusu usalama wa wagonjwa ndani ya kituo hicho. Hili ni tukio la pili katika kipindi cha chini ya miezi sita.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa muuguzi wa wodi hiyo alimpima Ndegwa saa tano na nusu asubuhi na kupima shinikizo la damu.

Saa kumi na mbili na nusu jioni, jamaa alimtembelea na kumkuta akiwa amepumzika.

Mgeni huyo aliondoka wodini mwendo wa saa moja na nusu usiku. Hata hivyo, takriban saa mbili usiku, mhudumu aliyekuwa akizunguka wodini aliona damu nyingi shingoni mwa mgonjwa.

“Walipofika eneo la tukio, wapelelezi waliona karatasi zenye damu kutoka kwenye kitanda cha mwathiriwa hadi kwenye choo kilicho karibu na hatimaye kwenye chumba cha pembeni, ambapo mshukiwa, Kalombotole, alilazwa,” DCI imesema katika taarifa .

“Katika chumba hicho, wachunguzi walipata jozi ya champali za bluu na shuka iliyotapakaa damu. Pia pale chini, moja kwa moja hadi ghorofa ya 7 lilipo dirisha la wodi ya marehemu, walipata kisu kilichokuwa kimefungwa kwenye glavu,” taarifa imeongezea.

Vitu zilivyopatikana vilipelekwa katika Maabara ya Kitaifa ya Uchunguzi.

Tukio hilo linakuwa ni la pili mwaka huu kwa mgonjwa kuuawa katika hospitali hiyo katika mazingira yasiyoeleweka. Mnamo Februari, mgonjwa mwingine alipatikana ameuawa ndani ya Hospitali baada ya kudungwa kisu na mtu asiyejulikana usiku wa Alhamisi, Februari 6.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Kennedy Kalombotole alilazwa katika kituo hicho mnamo Disemba 1, 2024, na ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji ya Gilbert Kinyua Muthoni, 40, aliyeuawa katika Wadi 7C usiku wa tarehe 6 na 7 Februari 2025.” taarifa ya DCI imeongezea.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#