Sport
Dollar
41,0483
0 %Euro
47,8689
0.02 %Gram Gold
4.475,0400
-0.07 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Licha ya Tanzania kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali, ikiwemo madini adimu kama nikeli na shaba, wachimbaji wa madini hayo kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kutonufaika ipasavyo.
Na Ronald Sonyo, TRT Afrika Dodoma
Changamoto hizi zinatokana na sababu kadhaa ikiwemo, uhaba wa viwanda vya uchenjuaji na kuyeyusha madini ili kuongezea thamani.
Hata hivyo, Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ya kukabiliana na changamoto hizo, kwa kujenga viwanda vipya na kuweka sheria kali inayokusudia kulinda wazalishaji wa ndani.
Hatua hizi zinakusudia kuhakikisha wachimbaji wananufaika moja kwa moja na rasilimali hizo.
Kwa sasa, miradi kadhaa ya viwanda vya kuongeza thamani ya madini ipo katika hatua za utekelezaji, ikiwemo kiwanda kitakachochakata zaidi ya tani 200,000 za nikeli na shaba kwa mwaka.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kusafisha na kusindika madini hayo kinachojengwa na Kampuni ya Zhongzhou Mining Co. Ltd, eneo la Zamahero, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, alisema Tanzania inalenga kuwa kitovu cha uchumi wa kijani, hasa katika kutengeneza magari ya umeme, betri za magari, nishati safi na vifaa vya kielektroniki.

“Ujenzi wa kiwanda hiki ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuongeza thamani ya madini nchini. Tunataka kuona Tanzania ikibadilika na kuwa taifa linalozalisha bidhaa zenye thamani kubwa kwenye soko la dunia la teknolojia,” amesema Mavunde.
Comments
No comments Yet
Comment