Sport
Dollar
40,6840
0.05 %Euro
47,5217
0.11 %Gram Gold
4.406,0400
0.07 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kulingana na taarifa iliyotolewa Agosti 5, 2025, Rais Samia pia amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.
Aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole amepoteza hadhi yake ya kidiplomasia, baada ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya nchi hiyo, ilisema kuwa imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka, ikitaarifu kwamba Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Polepole, aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba, na pia kumuondolea hadhi ya ubalozi.
Kulingana na taarifa iliyotolewa Agosti 5, 2025, Rais Samia pia amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.
Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu Julai 16, 2025.
Kupitia barua yake ya Julai 13, 2025, Polepole alitangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake ya kidiplomasia na uongozi wa umma, akitaja kukosekana kwa uelekeo sahihi katika uongozi wa kitaifa, kufifia kwa maadili na dhamira ya kuhudumia wananchi kama sababu kuu za hatua hiyo.
Comments
No comments Yet
Comment