Dollar

42,5354

0.07 %

Euro

49,5729

-0.06 %

Gram Gold

5.744,6300

-0.15 %

Quarter Gold

9.538,1500

0.27 %

Silver

79,8400

2.28 %

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema kuwa serikali imepokea kwa mshangao malalamiko ya kimataifa juu ya matukio ya Oktoba 29 licha ya mazungumzo ya wazi nao

Serikali ya Tanzania yashangazwa na taarifa ya nchi za kigeni juu ya matukio ya Oktoba 29

Serikali ya Tanzania imepokea na kushangazwa na taarifa na maoni ya umma yaliyotolewa kwa nyakati tofauti katika wiki iliyopita na washirika wa maendeleo na serikali kuhusu Tanzania na matukio ya 29 Oktoba 2025.

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya wizara ya mambo ya nje imeelezea kushangazwa na hamaki ya kimataifa licha ya kuwa tayari walishajieleza katika mkutano wa Novemba 29 kati ya serikali na waakilishi na mabalozi wa nchi hizo.

Taarifa hiyo inaomba watu wawe na subira hadi ripoti ya uchunguzi itakapotolewa.

‘‘Huku ikitambua nafasi ya jumuiya ya kimataifa katika kukuza demokrasia na maendeleo ya kijamii na kisiasa nchini, ni muhimu pia kutambua kuanzishwa kwa Tume ya Uchunguzi itakayofanya hivyo kuchunguza ghasia za baada ya uchaguzi na kutoa ripoti,’’ imesema taarifa.

‘‘Matokeo ya ripoti italeta uelewa wa matukio ya bahati mbaya yaliyotokea na
kuunda msingi wa ushirikiano wenye kujenga siku zijazo,’’ iliongeza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyowekwa saini na ‘kitengo cha mawasilianoi ya serikali‘ iliongeza kuwa, Serikali ya Tanzania inapenda kuwahakikishia jumuiya ya kimataifa na washirika wa maendeleo ya utayari wake na dhamira ya kuendelea kuhusika katika masuala yote yenye maslahi kwa pande zote, kama sawa washirika.

Hii inakuja baada ya zaidi ya nchi 17 za Ulaya kutoa taarifa ya pamoja ya kukemea ukatili uliotokea wakati na baada ya uchaguzi ambapo inakisiwa idadi kubwa ya watu waliuawa na kujeruhiwa kufuatia maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi.

Nchi hizo za Ulaya pia zimeitaka serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kurudisha miili ya vijana waliouawa katika machafuko hayo kwa familia zao kwa ajili ya maziko.

Rais Samia alijibu wito huo akieleza kuwa kuwa sio yeye aliyewatuma vijana kuandamana na hajui chochote kuhusu miili hizo.

Wiki chahce baada ya kutokea ghasia hizo za uchaguzi na malalamiko kutoka ndani na nje ya Tanzania, Rais Samia aliteua kamati maalum kufanyia uchunguzi rabsha hizo na ameahidi kuweka wazi na kufanyia kazi ripoti ya Kamati itakapotolewa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#