Dollar

41,2664

0.04 %

Euro

48,4290

-0.29 %

Gram Gold

4.841,9600

0.39 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania, unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, huku CCM kikimsimamisha kwa mara ya kwanza, mgombea mwanamke katika nafasi ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Samia: Chagueni mafiga matatu

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kukipigia kwa wingi, kura za ndio kwa nafasi ya Urais, Wabunge na Madiwani, akiifananisha dhana hiyo na mafiga matatu ya jiko.

Kulingana na Rais Samia, hatua hiyo yatawezesha kuweka urahisi wa kazi katika utekelezaji wa majukumu yao katika kuitekeleza vema ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/30.

Akizungumza na wananchi mkoani Singida, Rais Samia amesema kuwa iwapo atachaguliwa tena, basi serikali itakwenda kuendeleza kasi ileile ya uchapakazi wake.

 Wakati huo huo, mgombea huyo ameahidi kutatua tatizo la usikivu hafifu wa matangazo ya moja kwa moja ya TBC mkoani Singida.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#