Dollar

41,2757

0.06 %

Euro

48,4975

-0.14 %

Gram Gold

4.840,9100

0.37 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kinachojulikana kama uthibitisho wa kusikilizwa kwa mashtaka kinakuja miongo miwili baada ya ICC kutoa hati ya kukamatwa kwa Joseph Kony kwa madai ya uongozi wake wa kundi la kikatili la waasi.

ICC kuwasilisha ushahidi kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya Joseph Kony wa Uganda

Waendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, wataanza kuwasilisha ushahidi Jumanne ili kuunga mkono mashtaka yao dhidi ya kiongozi wa waasi wa Uganda Joseph Kony katika kesi ya kwanza kabisa ya kusikilizwa kwa mahakama hiyo ya kimataifa.

Kony, mwanzilishi na kiongozi wa kundi la Lord’s Resistance Army, au LRA, anakabiliwa na shutuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Mahakama hiyo inayoitwa uthibitisho wa kusikilizwa kwa mashtaka inakuja miongo miwili baada ya kutoa hati ya kukamatwa kwa Kony kwa madai ya uongozi wake wa kundi la kikatili la waasi ambalo lilijulikana kwa ukatili, ikiwa ni pamoja na kuwateka nyara watoto na kuwakata viungo mateka.

Usikilizaji wa kesi mbele ya ICC sio kesi halisi, lakini unaruhusu waendesha mashtaka kuelezea kesi yao mahakamani.

Kony atawakilishwa na wakili wa utetezi bila yeye mwenyewe kuwepo.

Baada ya kupitia ushahidi, majaji wanaweza kutoa uamuzi wa kuthibitisha au kutothibitisha mashtaka dhidi ya Kony, lakini hawezi kuhukumiwa isipokuwa akiwa chini ya ulinzi wa ICC.

Mashtaka dhidi ya Kony

Kony anakabiliwa na mashtaka 39 yakiwemo mauaji, utumwa wa kijinsia, ubakaji, na kuwasajili watoto askari, mashtaka yote yanayodaiwa kufanywa mwaka 2003 na 2004 kaskazini mwa Uganda.

Usikilizaji huo umeonekana kama kesi ya majaribio kwa mahakama kusonga mbele na kesi nyengine ambapo uwezekano wa kuwa na mshukiwa kizuizini unachukuliwa kuwa wa mbali, kama vile Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Kony apata umaarufu duniani mnamo 2012 wakati video kuhusu uhalifu wake iliposambaa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#