Uzinduzi huo umefanyika sambamba na ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), ambapo Rais Samia ameshiriki kama Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.

Rais Samia azindua Mwongozo wa Afya ya Mama na Mtoto barani Afrika

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, ambaye pia ni kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, amezindua Mwongozo wa Utekelezaji wa Kinara wa Umoja wa Afrika kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Watoto Wachanga, Watoto na Vijana katika Mkutano wa 5 wa Kimataifa wa Afya ya Umma barani Afrika (CPHIA 2026), unaofanyika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Uzinduzi huo, unatajwa kuwa hatua muhimu kwa wanawake, watoto na vijana barani Afrika, na wito wa kugeuza ahadi kuwa vitendo.

Uzinduzi huo umefanyika sambamba na ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), ambapo Rais Samia ameshiriki kama Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.

Mpango unaelekeza nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kufikia malengo matatu makuu, ambayo ni kuhakikisha kuwa, kila mwanamke anajifungua katika kituo cha huduma za afya akisaidiwa na mtaalamu, kukomesha vifo vinavyotokana na uzazi na vya watoto wachanga vinavyoweza kuzuilika na kuhakikisha kuwa, kila mtoto anapata chanjo.

TRT Afrika Swahili — TRT Afrika Swahili

Picha: Others

#