Dollar

42,9259

0.13 %

Euro

50,6303

-0.18 %

Gram Gold

6.252,4200

1.32 %

Quarter Gold

10.319,2000

1 %

Silver

108,1200

9.12 %

Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imetoa tamko kali kulaani jaribio lolote la kudhoofisha uhalali, usalama na umoja wa Somalia

Palestina yalaani na kukemea tamko la Israel kutambua Somaliland

Utawala wa Palestina umepinga vikali na kulaani kutambuliwa kwa Somaliland na taifa haramu la ukandamizaji la Israel.

Kupitia taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya nje kwenye mtandao wa X, Palestina imesema pia inapinga hatua zozote zinazounga mkono utengano au kudhalilisha uhalali wa Somalia , au zinazodhoofisha mamlaka na umoja wa Somalia na kuyumbisha usalama wake.

‘‘Wizara ya Mambo ya Nje ya Taifa la Palestina inathibitisha uungaji mkono wake kamili kwa umoja, mamlaka na uhuru wa kisiasa wa Somalia, na kuhakikisha haki ya watu wa Somalia ya maisha yenye heshima, usalama na utulivu, kulingana na sheria za kimataifa,’’ilisema taarifa hiyo.

Wizara hiyo ilisema kuwa utambuzi huo uliokataliwa unathibitisha majaribio ya Israel, kama nguvu ya kikoloni inayofanya kazi ya kudhoofisha amani na usalama wa kimataifa, haswa usalama wa kikanda na wa Kiarabu.

Taarifa hiyo ilishutumu Israel kwa kutishia eneo hilo na kuliweka katika hali ya kutokuwa na utulivu, kwa ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, Mkataba wa UN, na kanuni za kiutawala zinazohitaji kuheshimiwa kwa umoja wa nchi na nchi zao.

Awali Israel iliwahi kutaja Somaliland kama eneo linaloweza kutumiwa kuwahamishia Wapalestina, hasa kutoka Gaza.

‘‘Taifa la Palestina linathibitisha kukataa kwake kabisa mipango ya Israel ya kuwahamisha watu wetu kwa lazima, au kwa visingizio vingine vyovyote, na inachukulia kuwa ni mstari mwekundu,’’

Palestina pia imeonya dhidi ya taifa lolote kujifungamanisha na mtu yeyote na mapendekezo haya yaliyokataliwa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#