Dollar

40,4536

0.08 %

Euro

47,5219

-0.15 %

Gram Gold

4.448,7200

-0.21 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Ethiopia ilikuwa ikitumika kama kitovu muhimu cha siasa za kijiografia na kiuchumi kwa shughuli za kibiashara, biashara, na mwingiliano na mataifa kadhaa ya Asia na Ulaya.

Nini chanzo cha mvutano kati ya Ethiopia na Eritrea?

Eritrea ilikuwa sehemu ya Ethiopia, ambayo ilikuwa nchi kuu ya Bahari Nyekundu, na ilikuwa sehemu kuu ya biashara ya kimataifa.

Ethiopia ilikuwa ikitumika kama kitovu muhimu cha siasa za kijiografia na kiuchumi kwa shughuli za kibiashara, biashara, na mwingiliano na mataifa kadhaa ya Asia na Ulaya.

Bandari za Ethiopia, haswa Adulis wakati wa Milki ya Axumite na Asseb na Massawa katika karne ya 19, zilichukua jukumu muhimu katika kuunda uhusiano wa kimataifa wa Ethiopia.

Na bandari hizi mbili zinashikilia nafasi kubwa katika utambulisho wa kitaifa wa Ethiopia na jukumu lake la kimkakati katika siasa za kimataifa.

Mnamo 1993, Ethiopia ilikuwa nchi isiyo na bahari kufuatia kujitenga kwa Eritrea kutoka Ethiopia na kujipatia uhuru wake.

Mgogoro wa mpaka wa Ethio-Eritrea wa 1998-2000 ulibadilisha uhusiano wa Ethiopia na Eritrea kwa kuongeza tabaka kwa vipengele vyake tofauti.

Mgogoro huu kwa kiasi fulani ni matokeo ya uhasama wa kihistoria kati ya chama tawala wakati huo cha Ethiopia kilichoitwa Tigray People's Liberation Front na People's Front for Democracy na cha Eritrea kilichoitwa Justice (PFDJ), ambavyo vilijidhihirisha katika migogoro baina ya mataifa na mizozo ya mipaka.

Hata hivyo, mzozo huu wa miaka miwili ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 70,000. Baada ya mzozo huo mbaya, enzi ya "hakuna amani, hakuna vita" ilitawala.

Waziri Mkuu alipoingia madarakani 2018 aliahidi kumaliza uhasama huo.

Safari ya amani iliyoyumba

Makubaliano ya Jeddah yalimaliza uhasama huu na kufungua ukurasa mpya katika uhusiano kati ya Ethiopia na Eritrea.

Mahusiano kati ya serikali na nchi na watu, huduma za simu kurejeshwa, na usafiri wa anga ulianza tena, na mabadiliko ya kisiasa ya ndani nchini Ethiopia, yakianzishwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

Julai 8, 2018 Waziri Mkuu wa Ethiopai alifanya ziara hadi Asmara na hapo kumaliza uhasama wa zaidi ya miongo miwili kati ya nchi hizo.

Septemba 2019 Ubalozi wa Eritrea nchini Ethiopia ulifunguliwa upya.

Mwaka 2020 Eritrea iliunga mkono serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed wakati vita kati ya jeshi la taifa la Ethiopia na wanajeshi chini ya chama kilichokuwa kikitawala TPLF vilianza.

Wataalamu wa kisiasa wanasema ilikuwa rahisi kwa Eritrea kufanya hivyo kwani chama hicho cha TPLF ndicho kilikuwa kimefanya vita na Eritrea miongo iliyopita.

Lakini mwaka 2022 makubaliano ya amani yaliyofanyika Pretoria nchini Afrika Kusini baina ya Serikali ya Ethiopia na kikundi cha TPLF yaliiwacha Eritrea nje huku Ethiopia ikikubali kuwa majeshi ya eritrea yalikuwa yameingia kaskazini mwa nchi na ahta kuishutumua kwa kufanya uhalifu.

“Kilichojiri baada ya Mkataba wa Pretoria ni vigumu kufahamu. Kwa nini haukutekelezwa kwa nia njema? ” Rais wa Eritrea Isaias Afwerki alisema katika mahojiano yake na waandishi wa habari mjini Asmara.

Uhasama ukazuka upya

Ethiopia ilifanya makubaliano ya kupata ufuo wa bandari na Somaliland Januari 2024 Somalia ikapinga ikidai Somaliland haina haki ya kufanya hivyo.

Eritrea ikaonyesha kuwa karibu na Somalia, huku mikutano kadhaa kati ya marais hao wawili ikifanyika.

Rais Afwerki aliushutumu uongozi wa Ethiopia kwa kuingilia masuala ya Eritrea.

“Na kwa nini Chama cha Prosperity Cha Ethiopia kinachochea vita dhidi ya Eritrea badala ya kuzingatia, na kushughulikia matatizo yake ya nyumbani?” Rais aliuliza.

Juni 2025 Waziri Mkuu wa Ethiopia akihutubia bunge la nchi hiyo alikana kuwa Ethiopia haina nia ya vita na Eritrea.

“Ingawa masuala ambayo hayajatatuliwa yanasalia, lengo letu ni kukuza ushirikiano na kunufaishana. Utafutaji wetu wa kufikia bandari unatokana na mazungumzo ya amani na heshima kwa mamlaka, si kwa nguvu,” Waziri Mkuu Ahmed alisema.

Hatutafuti makabiliano na Eritrea au nchi nyingine yoyote—na tunatarajia vivyo hivyo kwa upande wao,” aliongezea.

Hata hivyo ametahadharisha.

“Ikiwa amani yetu itatishiwa, Ethiopia ina nguvu ya kujilinda. Licha ya changamoto za kihistoria zinazoendelea, Ethiopia itastahimili, kustawi, na kuendelea kusonga mbele.”

Eritrea nayo imejibu.

“Ujanja wa "ufikiaji huru wa bahari" una vipimo vingine vya kijiografia. Kuna nchi nyengine nyuma ya maneno haya. Lazima tukumbuke kwamba haki zetu za kuondoa ukoloni zilinyimwa miaka ya 1940 kwa visingizio sawa. Chama tawala cha Ethiopia kilielezea wakati mmoja nia ya kuelekeza bidhaa zake zote kutoka nje kupitia bandari ya Eritrea ya Assab huku ikiitelekeza Bandari ya Djibouti na hivyo kubatilisha mapato yake ya kila mwaka ya dola bilioni 4,” Rais Afwerki ameongezea.

“Tuliwaambia kwamba hatungekubali njama kama hiyo ya kudhuru nchi jirani. Mgawanyiko wao na uchochezi wa kupata bandari na kituo cha majini huko Somaliland na kadhalika unaangukia katika vitendo vile vile vya ukora,” ameongezea.

“Hatuna hamu ya vita. Lakini tumepigana vita miaka iliyopita. Hatuna madai ya eneo au matarajio dhidi ya majirani zetu. Lakini historia inavyothibitisha, tunajua jinsi ya kuilinda nchi yetu inaposhambuliwa,” ameongezea.

Wataalam wanasema uhasama kati ya nchi hizo mbili unaathiri zaidi wananchi wa kawaida ambao wallikuwa wamefurahia kufunguliwa kwa mipaka ya nchi hizo mbili na kukutana na jamaa na marafikia zao baada ya miongo kadhaa.

Mvutano huu sasa umeziba tena mipaka hiyo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#