Dollar

40,4503

0.08 %

Euro

47,5084

-0.13 %

Gram Gold

4.444,7300

-0.3 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Sehemu ya Chakama, inahusisha pia msitu wa Shakahola, ambako miili ya zaidi ya watu 450 ilifukuliwa kutoka makaburi mafupi mwaka 2023, katika tukio maarufu lililogusa hisia za wengi nchini Kenya.

Kenya: Polisi waanza uchunguzi baada ya  mafuvu mawili, mwili kufukuliwa huko Kilifi

Polisi nchini Kenya inawashikilia watu wanne huku wakiendelea na uchunguzi wa vifo vya watu, vinavyohusishwa na imani za kidini.

Vifo hivyo vinaripotiwa kutokea katika kijiji cha Binzaro kilichopo Chakama, Kaunti ya Kilifi.

Katika taarifa yake iliyotolewa siku ya Jumanne, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya imesema kuwa jeshi la polisi la nchi hiyo linaendelea na linaendelea kufanya uchunguzi kwenye nyumba tano ambazo zinahofiwa kuhusika na ibada hizo.

“Mtu mmoja mwenye miaka 50 ambaye taarifa yake ya kupotea kwake iliripotiwa katika kituo cha polisi cha Siaya toka Aprili 15, mke wake pamoja na wanawake wengine wawili wamepatikana katika boma hilo,” taarifa hiyo ilisema.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa, watu hao waliwekwa kwenye nyumba hiyo kwa ajili ya kufanyiwa ibada.

Mafuvu mawili ya binadamu na mwili wa mwanaume mmoja ilipatikana karibu na kichaka cha nyumba hiyo, kulingana na wizara hiyo.

Kulingana na wizara hiyo, mshukiwa mkuu, ambaye hakuweza kutambulika mara moja, tayari anashikiliwa na polisi, pamoja na watu wengine wanaohusika na tukio hilo.

Sehemu ya Chakama, inahusisha pia msitu wa Shakahola, ambako miili ya zaidi ya watu 450 ilifukuliwa kutoka makaburi mafupi mwaka 2023, katika tukio maarufu lililogusa hisia za wengi nchini Kenya.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#