Sport
Dollar
42,8554
0.06 %Euro
50,7250
0.06 %Gram Gold
6.178,0500
-0.24 %Quarter Gold
10.205,2300
0 %Silver
98,6200
0.12 %Televisheni hiyo ya AES imeelezwa katika mawasiliano rasmi kuwa chombo cha kukabiliana na upotoshaji wa taarifa na kuimarisha yanayojiri katika kanda hiyo.
Viongozi wa Muungano wa Mataifa ya Sahel (AES), kundi linalojumuisha Mali, Burkina Faso na Niger, umeanzisha shirika jipya la habari lenye makao yake makuu mji wa Mali, Bamako.
Televisheni ya AES inasemekana kuwa hatua muhimu katika malengo ya kutoa taarifa huru kwa kundi hilo la Afrika Magharibi, na limeelezwa kuwa chombo rasmi cha kukabiliana na upotoshaji wa taarifa na kuimarisha simulizi ya kanda hiyo.
Ilizinduliwa siku ya Jumanne na Rais wa Mali Jenerali Assimi Goita, Rais wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore na Rais wa Niger Jenerali Abdourahamane Tiani waliokutana mjini Bamako kwa mkutano wa siku mbili kutathmini mwaka mmoja wa muungano wa AES.
Mali, Burkina Faso na Niger walijiondoa rasmi kutoka kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) Januari 2025 kufuatia mchakato wa mwaka mzima.

Taarifa kutoka ofisi ya rais wa Burkina Faso inasema kuwa viongozi hao watatathmini ripoti ya utekelezaji, kufanya maamuzi ili kuangazia mafanikio na kushughulikia changamoto kubwa zinazokabili AES.
Traore pia alikuwa anatarajiwa kukutana na raia wa Burkina Faso wanaoishi Mali.
Hatua zilizopigwa na AES hivi karibuni ikiwemo uzinduzi wa kikosi cha pamoja cha AES wiki iliopita (FU-AES) ambacho kina makao makuu yake mjini Niamey. Kinategemewa kuwa na wanajeshi karibu 5,000 kukabiliana na makundi yenye silaha.

Kundi hilo lilianzisha Benki ya Uwekezaji na Maendeleo (BCID-AES), kwa mtaji wa kwanza wa CFA bilioni 500 billion (karibu dola milioni $900), kwa lengo la kupunguza utegemezi wa ufadhili kutoka nje kwa kuimarisha miundombinu, nishati na miradi ya kilimo.
AES, yenye kujumuisha watu milioni 78, inaendelea kuunganisha katika masuala ya usalama, uchumi na mawasiliano ishara ya kuelekea kujisimamia wenyewe katika eneo la Sahel.
Comments
No comments Yet
Comment