Sport
Dollar
42,8629
0.06 %Euro
50,7296
0.01 %Gram Gold
6.205,3100
0.2 %Quarter Gold
10.205,2300
0 %Silver
99,4800
0.99 %Mamlaka za nchini Uturuki zimesema kuwa mawasiliano yalipotea na ndege binafsi aina ya Falcon 50 iliyokuwa njiani kuelekea mjini Tripoli baada ya kutoa taarifa ya dharura karibu na katikati mwa Uturuki.
Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibeh ametangaza vifo vya mkuu wa majeshi na maafisa wengine wakuu kufuatia ajali ya ndege wakati wakirejea kutoka ziara rasmi nchini Uturuki.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, Dbeibeh alisema siku ya Jumanne amepokea taarifa hizo “kwa masikitiko makubwa na huzuni,” akithibitisha kufariki kwa Luteni Jenerali Mohammad al-Haddad na waliokuwa kwenye ujumbe wake.
Miongoni mwa wale waliofariki pamoja na al-Haddad ni mkuu wa majeshi ya ardhini, mkuu wa mamlaka za viwanda vya jeshi, mshauri wa mkuu wa majeshi, na mpiga picha wa ofisi ya habari.
Waziri mkuu amesema tukio hilo limetokea wakati wakirejea kutoka mji mkuu wa Uturuki Ankara, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu matukio hayo.
Akilitaja kuwa ni pigo kubwa kwa taifa na jeshi, waziri mkuu amesema Libya imepoteza watu waliokuwa wakitumikia nchi yao kwa nidhamu na dhamira kwa taifa,” akitoa salamu zake za rambirambi kwa familia, wafanyakazi wenzao jeshini na raia wa Libya kwa jumla.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya awali alisema mabaki ya ndege hiyo binafsi iliyokyuwa ikielekea Libya iliyombeba mkuu wa majeshi ya Libya iliondoka jijini Ankara yalikuwa yamepatikana katika wilaya ya Ankara ya Haymana.
Awali waziri huyo wa Uturuki alisema mawasiliano yalipotea na ndege hiyo iliyokuwa imembeba mkuu wa majeshi ya Libya muda mfupi baada ya kuondoka kutoka uwanja wa ndege wa Esenboga jijini Ankara.
Ndege hiyo ya kibiashara aina ya Falcon 50, yenye nambari 9H-DFJ, iliondoka saa mbili na dakika kumi usiku saa za Uturuki (1710 GMT) ikielekea mjini Tripoli. Mawasiliano yalipotea kama saa tatu kasoro dakika nane (1752 GMT), Yerlikaya alisema katika mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal.
Alieleza kuwa ndege hiyo ilitoa taarifa za kutaka kutuwa kwa dharura karibu na Haymana, wilaya iliyoko kusini mwa mji mkuu wa Uturuki Ankara.
“Hata hivyo, hakukuwa na mawasiliano zaidi na ndege hiyo baada ya ombi la awali la dharura,” alieleza.
Kulingana na waziri huyo, abiria watano walikuwa ndani ya ndege hiyo, ikiwemo al-Haddad.
Chombo cha habari cha Uturuki NTV kiliripoti kupotea kwa mawasiliano na ndege binafsi inayoaminika kumbeba al-Haddad katika anga ya mji mkuu, huku ufuatiliaji wa safari za ndege ukionesha ndege kadhaa zikiwa zimeelekezwa maeneo mengine mbali na Uwanja wa ndege wa Esenboga kama hatua ya tahadhari
Wizara ya Ulinzi ya Uturuki ilikuwa imetangaza mapema kuwa mkuu wa majeshi ya Libya alikuwa anafanya ziara jijini Ankara, ambapo alikutana na mwenzake wa Uturuki na makamanda wengine wakuu wa jeshi. Ziara hii ilikuwa sehemu ya ushirikiano wa kijeshi na kiusalama unaoendelea kati ya nchi hizi mbili.
Comments
No comments Yet
Comment