Sport
Dollar
42,8545
0.07 %Euro
50,7636
0.06 %Gram Gold
6.205,4700
0.2 %Quarter Gold
10.205,2300
0 %Silver
99,0000
0.5 %Shirika la Misaada la Ushirikiano na Uratibu la Uturuki (TİKA) limetoa mchango muhimu katika maendeleo ya jamii nchini Msumbiji unaolenga kusaidia wanawake, walionusurika vurugu.
Shirika la Misaada la Ushirikiano na Uratibu la Uturuki (TİKA) limetoa mchango muhimu katika maendeleo ya jamii nchini Msumbiji unaolenga kusaidia wanawake, ambao wamenusurika vurugu na dhulma za ngono.
Mradi huo unalenga kuwajumuisha katika maisha ya kijamii na kiuchumi.
Mpango huu wa misaada, ambao unawaleta pamoja walionusurika vurugu na dhulma za ngono chini ya mwavuli Shirikisho la Hixikanwe, unaangazia kuwawezesha kiuchumi.
Kama sehemu ya mpango huo, wana jiko la kisasa kwa ajili ya wanawake kuendeleza ujuzi wao kitaalamu wakati huohuo wakipata fursa ya kuingiza kipato kutokana na shughuli za eneo hilo.

Mfumo endelevu
Mradi huo pia unajumuisha kizimba kwa ajili ya kuuza vyakula.
Hii inatoa fursa kwa wanawake kutangaza kile wanachotengeneza, na kuwapa njia endelevu ya kuingiza kipato.
Kupitia mradi huu, TİKA inalenga kuwawezesha wanawake hao kiuchumi, kuimarisha uhuru wao, na kuunga mkono juhudi zao za kujihusisha na shughuli za kijamii.
Mradi huu siyo tu unatarajiwa kuchangia kwa shughuli ya kuwapa nafasi nyingine ya maisha lakini kwa jamii kwa upana kujumuisha katika masuala ya maendeleo.

Comments
No comments Yet
Comment