Dollar

41,3091

-0.13 %

Euro

48,6063

0.05 %

Gram Gold

4.842,0800

-0.07 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania (INEC) imemuondoa Luhaga Mpina kama mgombea urais kufuatia pingamizi dhidi yake iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Hamza Johari.

Mpina aondolewa tena kwenye mchakato wa  kugombea Urais

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Tanzania INEC imesema katika taarifa yake ya tarehe 15 Septemba kwamba, imeondoa jina la mgombea urais wa ACT Wazalendo Luhaga Mpina katika orodha ya wagombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 kufuatia pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo.

INEC imesema, awali ilipokea mapingamizi manne ambapo moja kati ya hayo ndilo lililokubaliwa na mengine matatu yamekataliwa.

"Tume imekubali pingamizi lililowasilishwa na Ndugu Hamza Saidi Johari, Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo," imesema taarifa ya Tume iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima R.K.

Pingamizi hili linakuja siku chache tu baada ya Mahakama Kuu nchini humo kusikiliza kesi ya hapo awali ambapo Mpina alikosa uteuzi wa Tume ya Uchaguzi kufuatia pingamizi la Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu uteuzi wake.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#