Sport
Mabadiliko hayo yanaonekana kuweka kipaombele katika uchumi, huku mchumi mwandamizi kutoka Benki ya Dunia Ahmed Rostom akiteuliwa Waziri wa Mipango, na mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Fedha Mohamed Farid Saleh akiteuliwa Waziri wa Uwekezaji.
Bunge la Misri siku ya Jumanne kwa asilimia kubwa limepitisha mabadiliko ya Baraza la Mawaziri wakati nchi hiyo ikipambana na kudorara kwa uchumi na shinikizo la migogoro ya kikanda.
Mabadiliko hayo yameathiri wizara 13, ikiwemo ya makazi, elimu ya juu, mawasiliano, vijana na michezo.
Hata hivyo, wizara muhimu kama ya mambo ya nje na ulinzi, hazijaguswa.
Wagombea walichaguliwa na Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri, ambae alikutakana na Waziri Mkuu Mustafa Madbouly mapema Jumanne, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais.
Mabadiliko hayo yanaonekana kuweka kipaombele katika sekta ya uchumi, huku mchumi mwandamizi kutoka Benk ya Dunia Ahmed Rostom akiteuliwa Waziri wa Mipango na mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Fedha Mohamed Farid Saleh akiteuliwa Waziri wa Uwekezaji.
Mawaziri wapya
Wakati huo huo, Wizara ya Habari imerudishwa tena baada ya kuondolewa mwaka 2021. Diaa Rashwan, mwenyekiti wa Huduma ya Habari ya Nchi, alitajwa kama waziri wake.
Mawaziri wawili wanawake pia walijumuishwa katika orodha mpya; Randa al-Menshawi hivi sasa anaongoza Wizara ya Makazi, na Gihane Zaki ameteuliwa Waziri wa Utamaduni.
Uchumi wa Misri kwa miaka mingi umekabiliwa na mabadiliko kadhaa kufuatia mpango wa Mfumo wa Fedha wa Kimataifa wa mwaka 2016, janga la corona, vita kati ya Urusi na Ukraine, na mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel huko Gaza.
Mashambulizi ya Houthi katika njia za meli katika Bahari ya Sham pia yamepunguza mapato ya Misri katika mfereji wa Suez Canal, sehemu kubwa ya mapato ya fedha za kigeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Kristalina Georgieva, ameiambia Sky News Arabia mwanzoni mwa mwezi huu kwamba Misri imeonesha dhamira ya mabadiliko katika uchumi na kwamba tathmini ya mwisho ya mpango wa mabadiliko ya uchumi wa Misri inakaribia kukamilika.
Hata hivyo, mabadiliko yameongeza gharama za maisha kwa raia wengi wa Misri, ikiwemo kuongezeka kwa bei ya mafuta na gharama za usafiri, huku thamani ya sarafu ya Misri ikipoteza thamani kidogo dhidi ya fedha za kigeni.
Takriban asilimia 30 ya raia wa Misri wanaishi katika umaskini, kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za serikali ya Misri.
Mwaka 2025, serikali ilipandisha kiwango cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi na kufikia pauni ya Misri 7,000 ($138), kutoka pauni 6,000 ($118.58).
Mara ya mwisho kufanyika kwa mabadiliko ya baraza la mawaziri ni Julai 2024.
Comments
No comments Yet
Comment