Dollar

38,8309

0.05 %

Euro

43,7144

-0.05 %

Gram Gold

4.023,8000

-0.15 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Biden, mwenye umri wa miaka 82, aligundulika kuwa na ugonjwa wa tezi dume baada ya kufanyiwa vipimo siku ya Ijumaa.

Mfalme Charles III wa Uingereza amtakia nafuu Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden

Mfalme Charles III wa Uingereza amemuandikia ujumbe wa kumtia moyo Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden ambaye amegundulika kuwa na ugonjwa wa tezi dume.

Mfalme Charles, ambaye pia anapokea matibabu ya ugonjwa wa saratani, limesema jumba la mfalme la Buckingham.

Biden, mwenye umri wa miaka 82, aligundulika kuwa na ugonjwa wa tezi dume baada ya kufanyiwa vipimo siku ya Ijumaa.

Ugonjwa huo unatajwa kusambaa kwenye mifupa.

Kupitia mitandao ya kijamii siku ya Jumatatu, Biden alionesha shukrani zake kwa watu waliomtakia heri na nafuu kwa maradhi yanayomsumbua.

"Ugonjwa huu unatugusa wote,” aliandika Biden.

Viongozi hao wamekuwa wakikutana mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.

Mwaka 2022, Biden aliitembelea uingereza wakati wa mazishi ya Malkia Elizabeth wa II, na kufanya mazungumzo na Charles, wakati akiwa bado ni mwana wa mfalme wa Wales – pembezoni mwa mkutano COP26 uliofanyika Glasgow mwaka 2021.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#