Dollar

38,7393

-0.06 %

Euro

43,5617

-0.23 %

Gram Gold

4.084,0700

-1.44 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Ukraine amekaribisha dalili ya uwezekano wa Urusi kumaliza vita na kuonyesha utayari wa mazungumzo ya amani ya ana kwa ana, kwa kuanza na usitishaji wa mapigano Mei 12.

Zelenskyy aona dalili njema huku Putin akiashiria kumaliza vita

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kwa tahadhari ameonyesha matumaini kufuatia ishara kwamba Urusi inaweza kufikiria kumaliza vita vinavyoendelea na Ukraine.

Katika taarifa ya Jumapili kupitia mtandao wa kijamii wa X, Zelenskyy ameielezea hali hiyo kama “ishara njema” ambayo inaweza kuwa mwisho wa mgogoro ulioiharibu  Ukraine na kugusa ulimwengu kwa zaidi ya mwaka.

“Ni ishara njema kwamba Urusi hatimae imeanza kufikiria kumaliza vita,” amesema Zelenskyy.

Ameongeza kusema kuwa dunia nzima inasubiri kuona ukatili umesitishwa, akisisitiza kwamba, hatua ya kwanza katika “kumaliza vita vyovyote ni usitishaji wa mashambulizi.”

“Tunatarajia Urusi kuthibitisha usitishaji wa mashambulizi-kikamilifu, na uhakika-kuanzia kesho, Mei 12, na Ukraine iko tayari kukutana,” amesema.

Kwa upande wake, Rais wa Marekani Donald Trump amesema katika mtandao wa kijamii wa Truth Social kwamba ataendelea kufanya kazi na pande zote mbili kuhakikisha usitishaji wa mapigano unatekelezwa.

Makubaliano ya Istanbul

Msaidizi wa masuala ya mambo ya nje ikulu ya Kremlin Yuri Ushakvo amesema Jumapili kwamba mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine yaliyopendekezwa na Rais Vladimir Putin yatazingatia hali ilivyo pamoja na majadiliano ya mwaka 2022, limeripoti shirika la habari za Interfax.

Putin Jumapili amependekeza mazungumzo ya moja kwa moja na Ukraine Mei 15 yatakayofanyika Istanbul.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#