Dollar

38,8502

0.08 %

Euro

43,7736

0.04 %

Gram Gold

4.030,5200

0.02 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Katika ziara yake, Fidan alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia Marko Djuric na viongozi wengine waandamizi katika ubalozi wa Uturuki ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo.

Mwanadiplomasia mkuu wa Uturuki akutana na Rais wa Serbia mjini Belgrade

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan siku ya Jumatatu, amekutana na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic wakati wa ziara yake jijini Belgrade, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imesema.

Baada ya kikao hicho, Vucic aliweka ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, akionesha kufurahia kikao chake na Fidan, akisisitizia umuhimu wa uhusiano kati ya Uturuki na Serbia kwa ajili ya utulivu wa kikanda.

Kulingana na Vucic, uhusiano wa nchi hizo mbili umejengwa kwenye misingi ya majadiliano na ushirikiano kwenye nyanja mbalimbali kama vile uchumi, nishati, utalii, utamaduni na elimu.

Pia, alipongeza utayari wa Uturuki katika kushiriki katika kongamano la kiulimwengu la mwaka 2027, litakalofanyika Belgrade, akisema kuwa ni hatua muhimu ya kukuza ushirikiano na maelelewano kati ya nchi hizo.

“Serbia inaipa umuhimu wa kipekee uhusiano wake na Uturuki, tukitambua nafasi yake katika utulivu wa kikanda,”alisema Vucic.

Katika ziara yake, Fidan alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia Marko Djuric na viongozi wengine waandamizi katika ubalozi wa Uturuki ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo.

Viongozi hao ni pamoja na mwenyekiti wa chama cha Social Democratic Rasim Ljajic, Usame Zukorlic kutoka chama cha haki na maridhiano, waziri wa maridhiano na uhusiano wa kikanda.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#