Dollar

41,2929

0.03 %

Euro

48,8204

-0.02 %

Gram Gold

4.840,3000

-0.34 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Haya yanajiri wakati Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema kuwa shirika hilo limepeleka tani 14 za vifaa vya matibabu, na vile vile kutuma watalaamu wa afya 48 katika kituo maalumu cha kushughulikia maradhi hayo nchini DRC.

Idadi ya vifo vya Ebola nchini DRC yafikia 31

Watu wapatao 31 wamethibitishwa kukutwa na maradhi ya Ebola kusini mwa DRC, tangu kuzuka kwa ugonjwa huo mwanzoni wa mwezi Septemba.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Brazzaville, afisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Patrick Otim, amesema kuwa kumekuwepo na maendeleo katika uchunguzi wa ugonjwa huo, toka ulivyoripotiwa Septemba 4.

“Ni wiki mbili sasa tangu ugonjwa huu uripotiwe. Kufikia sasa, tumethibitisha maambukizi 48,” alisema.

Kulingana na Otim, zaiid ya wagonjwa 15 wanapokea matibabu katika kituo maalumu kilichopo katika mji wa Bulape nchini humo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#