Dollar

40,6792

0.08 %

Euro

47,0721

-0.2 %

Gram Gold

4.392,1900

-0.07 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Ghana, John Dramani Mahama, anawataka jamii ya kimataifa kuhakikisha ulinzi wa maisha nchini Palestina na kutoa msaada muhimu wa kibinadamu.

Ghana yatoa msaada wa kibinadamu kwa Palestina

Rais wa Ghana, John Dramani Mahama, ametoa tani 40 za msaada wa kibinadamu kwa ajili ya kupelekwa Palestina, ambako vita vinavyoendelea vya kikatili vya Israel vimesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 60,000 huko Gaza huku njaa ikizidi kuenea.

Msaada huo, ukiwemo bidhaa za kakao zinazozalishwa Ghana, ulipokelewa na balozi wa Palestina nchini Ghana, Abdul Fattah Ahmed Khalil al-Sattari, ambaye alitoa shukrani za dhati.

‘‘Tunashukuru kwa msaada huu. Sote tunajua kwamba huko Gaza sasa kuna njaa na mauaji ya kimbari,’’ alisema Balozi al-Sattari.

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo iliyofanyika Accra siku ya Ijumaa, Rais Mahama alilaani mauaji yanayoendelea Gaza yanayofanywa na Israel pamoja na kulaani ukimbizi wa Wapalestina.

Ghana inaunga mkono suluhisho la mataifa mawili.

''Msaada huu wa chakula ni wa ishara na wa vitendo. Ni wa ishara kwa sababu kakao ni moja ya bidhaa za thamani kubwa za Ghana. Ni wa vitendo kwa sababu kakao ni chakula chenye nguvu kubwa,'' shirika la habari la Ghana lilimnukuu rais akisema.

''Tunatumaini kwa dhati kwamba bidhaa hizi za kakao zitatoa faraja, lishe, na ishara ya mshikamano wetu kwa familia zinazokumbwa na hali ngumu isiyoweza kufikirika,’’ alisema Rais Mahama.

''Ni kwa maslahi yetu ya pamoja kama jamii ya kimataifa kuhifadhi maisha, kulinda utu, na kushikilia misingi ya haki na amani,'' aliongeza.

''Kwa hivyo, tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutokata tamaa katika kuunga mkono juhudi zote za kufanikisha amani na utulivu katika eneo hilo na kutoa msaada muhimu wa kibinadamu kwa wale walioathirika.''

Rais Mahama alisisitiza tena msaada wa nchi yake kwa suluhisho la mataifa mawili.

''Tunasimama imara katika kuunga mkono suluhisho la mazungumzo ya mataifa mawili kwa suala la Palestina. Hii ni kwa mujibu wa sheria za kimataifa na maazimio husika ya Umoja wa Mataifa,'' alisema kiongozi wa Ghana.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#