Hii ni mara yake ya pili kuja Tanzania baada ya kusimamia Klabu pinzani ya Simba SC

Fadlu Davis atua Yanga kama kocha wao mpya

Mabingwa wa Tanzania, Young Africans, wamemteua mtaalamu kutoka Afrika Kusini, Fadlu Davids, kuwa kocha wao mkuu mpya, akichukua nafasi ya raia mwenzake, Manqoba Mngqithi.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 anarejea nchini Tanzania baada ya kufanya kazi na wapinzani wao, Simba SC, pamoja na klabu ya Raja Casablanca ya Morocco.

Akiwa na Simba, Davids aliiongoza klabu hiyo kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2024/25, ambapo walipoteza dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Sasa anakabiliwa na jukumu la kurejesha utawala wa Yanga katika mashindano ya ndani, huku klabu hiyo ikiwa nyuma ya Simba kwa pointi tano kwenye ligi baada ya michezo kumi.

Pia, anatarajiwa kuimarisha kampeni ya Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), ambapo watakabiliana na Zamalek, MC Alger, na Club Africain katika hatua ya makundi.

TRT Afrika and agencies — TRT Afrika and agencies

#