Sport
Dollar
40,6777
0.05 %Euro
47,5831
0.15 %Gram Gold
4.417,3700
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Baada ya zoezi hilo kusimamishwa mwaka 2022 kutokana na ukiukaji wa mkataba na mshirika wa zamani, mradi huo sasa unaanza upya huku ushirikiano mpya ukikamilika na kampuni ya kutoka Ghana.
Kama sehemu ya ufuatiliaji wa mageuzi ya kipaumbele ya Mkuu wa Nchi, Baraza la Rais la Ufuatiliaji wa Kimkakati (CPVS), linaendelea na juhudi zakutoa vitambulisho vya taifa kwa raia.
“Miongoni mwa mambo hayo, mchakato wa kutoa kitambulisho cha taifa ni hatua kubwa,” serikali ya DRC imesema.
Baada ya kusimamishwa mwaka 2022 kutokana na ukiukaji wa mkataba na mzabuni wa zamani, mradi huo sasa unaanza upya huku ushirikiano mpya ukikamilika na kampuni ya kutoka Ghana.
“Mageuzi haya yanaashiria hamu kubwa ya Rais kumpa kila Mkongo utambulisho wa kisheria, unaoaminika na kuweka msingi wa sera yoyote ya ujumuishi, usalama na maendeleo,” serikali imesema.
Jaribio la kwanza la kadi kwa raia 700 limekamilika kwa mradi wa majaribio katika mji mkuu wa Kinshasa.
Ili kujua wanaohitaji kitambulisho, serikali inasema itatumia sensa ya taifa pamoja na kuweka matabaka mbali mbali ya watu, kwa mfano wanafunzi, wanajeshi, raia walio ng'ambo na wakimbizi.
“Zaidi ya ofisi 5,000 za kudumu zitawekwa kote nchini kutoa huduma hii na kadi itatolewa bure,” serikali imesema.
Ada itatozwa tu iwapo mtu atapoteza kitambulisho chake na kutafuta chengine au mtu kuamua kutoa kipya baada ya cha zamani kuharibika.
Comments
No comments Yet
Comment