Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza hali ya dharura katika maeneo yalioathirika na dhoruba hiyo, ambayo iliharibu majengo zaidi ya 17,000 na paa zaidi ya 8,500 za nyumba katika mkoa wa kusini wa Masvingo.

Dhoruba yaharibu paa 8,500 za nyumba kusini mwa Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza hali ya dharura katika maeneo yalioathirika na dhoruba hiyo, ambayo iliharibu majengo zaidi ya 17,000 na paa zaidi ya 8,500 za nyumba katika mkoa wa kusini wa Masvingo.

"Kufuatia dhoruba kali iliyotokea mkoa wa Masvingo Jumatatu jioni, Oktoba 5, 2026, Rais Mnangagwa alitangaza hali ya tahadhari katika maeneo yaliyoathirika," Waziri wa Serikali za Mitaa na Ujenzi Daniel Garwe alisema katika taarifa.

"Hali mbaya ya hewa imeharibu majengo kote katika maeneo ya makazi ya watu, sehemu muhimu za umma, taasisi za elimu na afya, na maeneo ya biashara, kufanya iwe muhimu kutafuta hatua za kutafuta suluhu ili kulinda maisha ya watu na kusaidia katika ujenzi upya," Garwe aliongeza.

Kulingana na serikali, shughuli za biashara katika mji wa Masvingo zilitatizwa kutokana na dhoruba kubwa, iliyosababisha kukatika kwa umeme.

Hakuna aliyefariki: serikali

Maeneo kadhaa ya elimu, vituo vya afya, na sehemu za burudani paa ziliharibika sana, kusababisha maji kuvuja na majengo kuwa na nyufa.

Serikali ya Zimbabwe inasema hakuna aliyefariki, ingawa idadi ya waliojeruhiwa ilikuwa bado inafanyiwa uchunguzi.

#