Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Watafiti waliopitia kumbukumbu mbalimbali, wanadai kuwa benki hiyo iliwezesha kufanyika kwa miamala kadhaa ya fedha kwa ajili ya serikali ya Rwanda mwanzoni mwa miaka ya 1990, ikiwa ni maandalizi ya mauaji hayo ya kimbari.
Wanaharakati wa haki za kibinadamu na watafiti mbalimbali wameituhumu Benki Kuu ya Ufaransa kwa kuhusika kwa namna moja katika matukio yaliyopelekea kutokea kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya jamii ya Kitutsi.
Madai hayo yaliwasilishwa na wanasheria Matilda Ferey na Joseph Breham kwa niaba ya Dafroza na Alain Gauthier pamoja na taasisi ya CPCR.
Watafiti waliopitia kumbukumbu mbalimbali, wanadai kuwa benki hiyo iliwezesha kufanyika kwa miamala kadhaa ya fedha kwa ajili ya serikali ya Rwanda mwanzoni mwa miaka ya 1990, ikiwa ni maandalizi ya mauaji hayo ya kimbari.
Kulingana na wasilisho hilo, inawezekana kuwa benki hiyo ilishindwa kuzuia au ikaendelea kuidhinisha pesa, licha ya tahadhari kadhaa kutoka jumuiya mbalimbali za kimataifa kuhusu mzozo wa Rwanda.
Malalamiko hayo yaliegemea zaidi kwenye miamala saba iliyofanywa kutoka kwenye akaunti ya Benki ya Taifa ya Rwanda, iliyofanyika kati ya mwezi Mei na Agosti 1994.
Miamala hiyo inakadiriwa kufikia Dola 570,942, ambazo zinadaiwa kutumika kununua vifaa vya kijeshi na silaha, licha ya zuio la Mei 17, 1994 kutoka kwa Umoja wa Mataifa.
Comments
No comments Yet
Comment