Sport
Dollar
42,6208
0.05 %Euro
50,0704
0.44 %Gram Gold
5.771,5000
-0.38 %Quarter Gold
9.508,3700
0.04 %Silver
85,4000
0.91 %Mhagama ametumikia nyadhifa mbalimbali ikiwemo kuwa waziri katika awamu mbalimbali.
Mbunge wa Jimbo la Peramiho nchini Tanzania, Jenista Joakim Mhagama amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58.
Taarifa za kifo cha mwanasiasa huyo ambae amewahi kutumikia serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ile ya Waziri wa Afya mwishoni mwa serikali ya awamu ya sita kipindi cha kwanza zimetolewa na Spika wa Bunge la nchi hiyo Mussa Azzan Zungu siku ya Alhamisi huko jijini Dodoma nchini Tanzania.
Spika Zungu amesema msiba huo ni pigo kwa taifa.
"Natuma salamu zangu za rambirambi kwa familia, marafiki na wakazi wa Peramiho," Spika Zungu alisema akiwa Bungeni.
Kwa upande wake, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania nae ameungana na wabunge katika kuomboleza msimba huo na kutuma salamu zake za rambirambi kwa Spika wa Bunge na familia yake.
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama. Ninatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu, wananchi wa Jimbo la Peramiho, familia, ndugu, jamaa na marafiki."
Mhagama ametumikia nyadhifa mbalimbali ikiwemo kuwa waziri katika awamu mbalimbali.
Comments
No comments Yet
Comment