Dollar

42,6137

0.03 %

Euro

50,1966

0.66 %

Gram Gold

5.843,6800

0.87 %

Quarter Gold

9.503,9100

-0.01 %

Silver

86,9600

2.76 %

Hatua hiyo inakuja siku mbili baada ya Rais Felix Tshisekedi wa DRC kudai kuwa Rwanda ilikuwa ikienda kinyume na mkataba ‘Washington Accord’.

Rwanda yazilaumu DRC na Burundi kwa kukiuka mkataba wa amani wa Washington

Rwanda imeyanyooshea majeshi ya DRC na Burundi kidole cha lawama, kwa kile inachokiita ukiukwaji wa usitishwaji wa mapigano, kama ulivyowekwa bayana kwenye mkataba wa amani uliosainiwa Disemba 4, 2025 nchini Marekani.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo na Nje ya Rwanda ilisisitiza kuwa haitokuwa tayari kuwajibishwa kwa matukio yanayoendelea Kusini mwa Jimbo la Kivu.

Rwanda imeyatuhumu majeshi ya DRC na Burundi pamoja na wanamgambo wengine, kwa madai ya kuvishambulia vijiji vilivyo karibu na mpaka wa Rwanda kwa kutumia ndege za kivita.

Taarifa ya Rwanda inakuja inakuja siku mbili baada ya Rais Felix Tshisekedi wa DRC kudai kuwa Rwanda ilikuwa ikienda kinyume na mkataba ‘Washington Accord’.

Jeshi la Burundi linadaiwa kukusanya vikosi vya wapiganaji wapatao 20,000 katika eneo la Kusini la Kivu kwa lengo la kuiunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuvishambulia vijiji vya Banyamulenge vilivyopo Minembwe, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#