Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Tayari mamia ya wananchi wamefunguliwa mashtaka kwa makosa ya jinai huku viongozi wa upinzani wakiwekwa kwenye orodha mpya ya watakaokamatwa na kushtakiwa

Amaan Golugwa akamatwa huku polisi Tanzania ikiwasaka viongozi wa upinzani kufuatia maandamano

Naibu Katibu Mkuu Bara wa CHADEMA Amani Golugwa amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha Jumamosi asubuhi.

Taarifa ya kukamatwa kwake imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia ambaye pia ametajwa katika orodha ya wanasiasa wa upinzani wanaosakwa na polisi Tanzania kwa madai ya kuchochea maandamano yaliyoishia kwa ghasia na vifo.

‘‘Kukamatwa kwa Naibu katibu Mkuu kunaamisha kwamba serikali imewaacha nje viongozi watatu tu kati ya sita wa chama,’’ ilisema taarifa ya CHADEMA iliyochapishwa mtandaoni.

Mamlaka ya Tanzania iliwashtaki mamia ya watu kwa kosa la uhaini kutokana na maandamano hayo katika uchaguzi uliozozaniwa mwezi uliopita, katika hali iliyozidisha mvutano wa kisiasa.

Mbali na makumi ya mashitaka ya jinai siku moja mapema jijini Dar es Salaam, makumi ya wengine wanakabiliwa na mashtaka kama hayo ya uhaini mahali pengine katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kulingana na rekosi za mahakama ambazo zilipatikana hadharani Jumamosi.

‘‘Tunaelewa kuwa serikali ina mpango wa kuwakamata na kuwapa kesi ya uhaini viongozi wetu ili chama kikose viongozi wa kukiendesha na kipoteze uelekeo,’’ alisema Naibu Katibu Mkuu Brenda Rupia.

Polisi pia walitoa vibali vya kukamatwa kwa baadhi ya maafisa wakuu wa upinzani ambao walikuwa bado hawajafungwa.

Viongozi wa kisiasa wanaosakwa

Hao ni pamoja na Brenda Rupia, mkurugenzi wa mawasiliano wa chama cha upinzani cha Chadema, pamoja na John Mnyika, katibu mkuu wake. Chadema ni chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Kiongozi wake, Tundu Lissu, amefungwa kwa miezi kadhaa na pia anakabiliwa na mashtaka ya uhaini baada ya kuhimiza mageuzi ya uchaguzi kabla ya kupiga kura Oktoba 29.

CHADEMA, wala viongozi hao binafsi hawakupatikana mara moja kuzungumzia taarifa hiyo ya polisi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#