Dollar

43,0429

0.14 %

Euro

50,7085

0.13 %

Gram Gold

6.043,3900

1.29 %

Quarter Gold

10.158,3200

0 %

Silver

101,0900

2.17 %

‘Kama Israel inajiweka katika maeneo ya watu kushambulia sehemu za watu wengine, basi hao watu pia watashambulia Somaliland na Somalia,’ rais wa Somalia ameonya baada ya Israel kutambua eneo lililojitenga.

‘Hatutaki Israel ituletee matatizo,’ rais wa Somalia anasema

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud anasema nchi yake haitaki Israel kuwepo Somaliland, akionya kutambua kwa Israel kwa eneo lililojitenga kunahatarisha kuleta mgogoro kwenye kanda hiyo.

“Hatujawahi kushambulia Israel. Hatujawahi kuwaletea matatizo Israel. Hatutaki Israel waje kwetu na kutuletea matatizo,” Mohamud aliliambia shirika la habari la Uturuki TRT World katika mahojiano ya kipekee.

Alieleza hatua hiyo kama “hali mbaya sana,” akitoa wito wa kuheshimiwa kwa sheria ya kimataifa.

Mohamud alisema hatua za hivi karibuni za Israel “siyo sahihi na hazirandani” na sheria ya kimataifa, akieleza kuhusu Gaza na historia ndefu ya mgogoro wa Mashariki ya Kati.

“Ni masikitiko makubwa kwamba sasa hilo limehamishiwa nchini Somalia,” alilalamika.

Uungwaji mkono duniani

Mohamud amesema Somalia imekuwa ikiwasiliana na jamii ya kimataifa, ikiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, IGAD, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu, na Muungano wa Ushirikiano wa Mataifa ya Kiislamu, ambayo yote yameungana na Somalia na kutangaza wazi kuunga mkono uhuru wa mipaka yao.

Alisema maeneo ya kaskazini mwa Somalia yamekuwa yakikabiliwa na changamoto za kutaka kujitenga kwa muda mrefu, lakini serikali imekuwa ikitaka kutatua tofauti zao kwa njia ya amani.

“Serikali ya Somalia haijawahi kuwalazimisha au kupigana nao, au hata kutumia uwezo wa kidiplomasia dhidi ya watu hawa,” aliongeza.

Mohamud alisema Uturuki imejaribu kupatanisha kati ya Somaliland na Somalia, kwa kufanya mikutani 2015 na kuwepo na mwakilishi mjini Hargeisa ili kuendelea na majadiliano.

Uturuki kwa kawaida imekuwa ikiunga mkono Somalia, Mohamud alisema, kila wakati ikiunga mkono umoja wake na uhuru wake kipindi cha changamoto hizo.

Uturuki “daima” imekuwa pamoja na watu ambao wananyimwa haki zao, aliongeza.

Kutambuliwa kunaweza kusababisha mgogoro zaidi

Mohamud alisema kuwa Somalia inaungwa mkono na jamii ya kimataifa licha ya Israel kuitambua Somaliland.

Kiongozi huyo wa Somalia alisema suala hilo ni muhimu kutokana na matukio ya Israel ya hivi karibuni Mashariki ya Kati, siyo tu kwa Palestina lakini pia kwa Syria na Lebanon, kuwa na hali ya wasiwasi kuhusu kujihusisha kwao katika Bahari ya Shamu, Ghuba ya Aden, na Pembe za Afrika, ambayo amelitaja “kuwa hali tete sana”.

Alisema kuwepo kwa Israel kunaweza kusababisha mapigano kuregea katika baadhi ya maeneo nchini Somalia na kwa nchi jirani katika Ghuba ya Aden na Ghuba ya Arabuni, akieleza kuwa Wahouthi wa Yemen na Iran pia wana uhusiano mbaya na Israel.

“Kama Israel inajiweka katika maeneo ya watu kushambulia sehemu za watu wengine , basi watu hao pia watashambulia maeneo ya Somaliland na Somalia, ambalo halitakuwa jambo zuri,” Mohamud ameonya.

Amesema kuwekwa kambi ya kijeshi Somaliland na kulazimisha kuwaondoa Wapalestina kunaweza kusababisha mzozo zaidi, hatua ambayo serikali ya Somalia na watu wake wameikataa kabisa.

Mapema, Mohamud aliliambia shirika la habari la Qatar Al Jazeera kuwa Somaliland imekubali kuwapokea Wapalestina, kuwa na kambi ya kijeshi ya Israel, na kujiunga na makubaliano ya pamoja na nchi za kiarabu na wao watambuliwe na Israel, kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia.

Uhusiano wa Somalia na Uturuki

Rais wa Somalia alieleza kuhusu ushirikiano wa kimkakati na Uturuki, akisema kuwa ushirikiano wao ni katika sekta ya ulinzi, usalama, uwekezaji, raslimali asilia, bandari, na “Uchumi unaotokana na bahari.”

Amesema katika siku za hivi karibuni alimpa taarifa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuhusu maendeleo ya Somalia juu ya usalama, demokrasia, na ujenzi wa taifa, na kujadili kuhusu miradi ya pamoja.

Mohamud amesema uwekezaji wa moja kwa moja wa mataifa ya kigeni “bila shaka” utafanyika Somalia.

Uwekezaji wa Uturuki umefungua soka la Somalia kwa uwekezaji wa moja wa moja kutoka kwa mataifa ya nje, hasa katika sekta ya mafuta na gesi, na kwamba Somalia inatarajiwa kuwa taifa la kuzalisha mafuta, aliongeza.

“Pia utakuwa wakati mzuri kwa Uturuki kuzalisha mafuta kwa kutumia teknolojia yake wenyewe, siyo kwa teknolojia iliyoletwa au kukodishwa kutoka sehemu nyingine,” alisema.

Mohamud alisema ushirikiano wao utafaidi mataifa yote mawili kiuchumi na kidiplomasia, kuwapa Uturuki fursa nzuri katika sekta ambayo inahitaji uwekezaji wa muda mrefu na ambao haitabiriki.

Uturuki pia ilikamilisha tathmini ya muundo wa kituo cha anga ambacho kitajengwa Somalia na tayari awamu ya kwanza ya ujenzi huo imeanza.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#