Kulingana na Waziri wa Habari ya Zimbabwe, matokeo ya uchunguzi huo, yatawekwa hadharani.
Serikali ya Zimbabwe imesema kuwa uchunguzi wa ajali ya helikopta iliyokuwa imembeba mfanyabiashara maarufu nchini humo, Wicknell Chivayo na mkewe, itahusisha wataalamu kutoa timu za kimataifa.
Kulingana na Waziri wa Habari wa nchi hiyo, Zhemu, uchunguzi wa awali umeshakamilika ambapo, mabaki ya helikopta hiyo, yamehifadhiwa katika eneo maalumu kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ambao utahusisha wataalamu wa kimataifa.
Aliongeza kuwa, timu hiyo ya wachunguzi, itatafuta ukweli kujua chanzo cha ajali hiyo, iliyochukua uhai wa Chivayo na mkewe, pamoja na watu wengine watatu, wiki iliyopita.
Chivayo, maarufu pia kama “Sir Wicknell”, alifariki dunia, yeye pamoja na mkewe, Lucy Muteke, baada ya helikopta binafsi waliyokuwa wakisafiria, kuanguka katika eneo la vijijini la Marondera, nchini Zimbabwe.
Wawili hao, wanatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamisi, katika makaburi yaliyopo jijini Harare,
