Matokeo hayo, yanaifanya Young Africans kufikisha alama 5, ikishuka hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi B kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Young Africans ya Tanzania njia panda kutinga Robo Fainali ya CAF

Mashabiki wa Klabu ya Young Africans ya Tanzania, sasa watakuwa wanapiga mahesabu ya namna gani wataingia hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa AS FAR Rabat ya nchini Morocco, Februari 7, 2026.

Matokeo hayo, yanaifanya Young Africans kufikisha alama 5, ikishuka hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi B kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa sasa, Young Africans, itakuwa ikipigia mahesabu mechi zake za mwisho, ili kujua hatma yake ijayo.

Ili iwe na nafasi ya kuingia hatua ya Robo Fainali, Young Africans inapaswa kushinda mchezo wake wa mwisho kwenye kundi hilo, na kuiombea AS FAR ipoteze mchezo wake.

Katika mchezo  huo wa Februari 7, 2026, bao lililotatiza matumaini ya Young Africans, lilifungwa na Anas Bach katika dakika ya 85, baada ya walinzi wa timu hiyo ya Tanzania, kujichanganya wakati wa kuokoa hatari, na mpira kumkuta mfungaji aliyeachia shuti ndani ya boksi, huku kipa Djigui Diarra akishindwa kuzuia mchomo huo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#