Dollar

38,8949

0.36 %

Euro

43,4533

-0.25 %

Gram Gold

3.997,1000

-0.9 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Martha Karua, mwanasiasa mkongwe wa upinzani kutoka Kenya pamoja na wenzake wadaiwa kurejeshwa walikotoka, bila sababu kutolewa japo wanadai kuwa walikuwa wageni wa chama cha wanasheria Tanzania.

Wana vuguvugu wa upinzani kutoka Kenya wazuiwa kuingia Tanzania


Kiongozi wa chama cha upnzani nchini Kenya, PLP Martha Karua ameweka video mtandaoni kudai kuwa yeye na wageni wengine wa Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki walizuiwa kuingia Tanzania bila kuelezewa sababu.

Katika video hiyo ya dakika moja, Martha Karua anaonekana na wenzake wengine wawili wakilalamika kuwa wamezuiliwa katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es alaam baada ya kuwasili mwendo wa asubuhi, Jumapili.

‘‘Tupo katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Daresalaam ambapo sote watatu tumezuiliwa na tunasubiri kurejeshwa Kenya,’’ anasema Martha Karua. ‘‘Tulidhani kama wananchi wa Afrika mashariki tulikuwa huru, lakini naona bado hakuna uhuru,’’ anaongeza kusema katika video.

Japo hawakuelezewa sababu za kuzuiliwa, Martha Karua na wenzake wanaonekana kucheka katika video ishara kwamba hawakunyanyaswa.

Madai ya uhusiano na upinzani

Japo wameweka wazi kuwa hawakuelezewa sababu za kuzuiwa kuingia Tanzania, Martha Karua ameendelea kutoa malalamiko kuwa huenda kuzuiliwa kwao ni kutokana na kuhusishwa na kesi inayomkabili kiongozi wa chama cha upinzani CHADEMA, Tundu Lissu.

‘‘Kuna woga katika serikali hii ya Mama wetu mpendwa Suluhu Hassan, dhidi ya yeyote anayeonyesha kufuatilia kesi inayomkabili Tundu Lissu. Aluta Kontinua,’’ Karua na wenzake wanaonesha ishara ya upinzani mwishoni mwa video.

Martha Karua, ambaye binafsi ni mwanasheria, si mgeni katika madai ya kujihusisha na kesi za hali ya juu kisiasa katika nchi jirani.

Mapema mwaka huu, amekwaruzana na vyombo vya sheria nchi jirani ya Uganda, aliponyimwa ruhusa kumwakilisha kiongozi wa upinzani Kizza Besigye ambaye kesi yake ya uhaini dhidi ya serikali bado inaendelea.

Amekuwa wazi pia juu ya msimamo wake kuhusu kesi inayomkabili kiongozi wa CHADEMA Tundu Lissu anayodai imechochewa kisiasa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#