Sport
Dollar
41,2417
0.14 %Euro
48,4184
0.58 %Gram Gold
4.760,4500
1.46 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Uhalifu dhidi ya binadamu wa wapiganaji wa RSF ni pamoja na mauaji ya halaiki, dhulma za ngono, uporaji, na uharibifu wa maisha ya watu, wakati mwingine ikiwa pamoja na mateso na uangamizaji.
Wapiganaji wa Rapid Support Forces wametekeleza uhalifu dhidi ya binadamu wakati wakizuia watu kuondoka El-Fasher jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulisema siku ya Ijumaa.
Wanaotekeleza zaidi uovu huu ni RSF katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinaingia mwaka wake wa tatu sasa, ujumbe huo ulisema kwenye ripoti yake ambayo ilisisitiza uchunguzi uliofanyika hapo awali.
"RSF pia imefanya uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mauaji ya watu wengi, dhulma za kingono, uporaji, na uharibifu wa maisha ya watu— wakati mwingine ikiwa ni pamoja na mateso na uangamizaji wa watu," mwenyekiti wa ujumbe, Mohamed Chande Othman, alisema katika taarifa.
Kuzuia watu kutoka
Kamati hiyo ya watu watatu ya Umoja wa Mataifa imepewa majukumu na Baraza la Haki la Binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza ukiukwaji huo wa haki.
Comments
No comments Yet
Comment