Dollar

41,2417

0.14 %

Euro

48,4168

0.58 %

Gram Gold

4.760,3300

1.46 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa kikosi kazi cha dharura kilichoundwa baada ya mlipuko kimeshauri kuwa hali hiyo siyo ya dharura ya kimataifa tena

Mlipuko wa Mpox Afrika siyo suala la dharura duniani tena - WHO

Shirika la Afya Duniani halichukulii tena mlipuko wa mpox barani Afrika kuwa dharura ya kiafya kimataifa, mkurugenzi wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa alisema siku ya Ijumaa.

Aina mpya ya mpox iliibuka mapema 2024 Congo na mataifa jirani ya barani Afrika, ikiambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ikiwemo kujamiiana. WHO ilisema ilitangaza maambukizi hayo kuwa dharura ya kiafya duniani Agosti mwaka jana.

Mkurugenzi Mkuu Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa kuwa kikosi kazi cha dharura kilichoundwa baada ya mlipuko kimeshauri kuwa hali hiyo siyo tena dharura kimataifa, na “Nimekubali ushauri wao.”

Tangazo la dharura ya kimataifa la WHO, idara ya juu zaidi ya kuonya kuhusu tishio la masuala ya afya, linaashiria kutolewa kwa raslimali na kuhamasisha umma miongoni mwa hatua nyingine.

‘Tishio bado lipo’

“Bila shaka, kuondolewa kwa tangazo la dharura haimanishi tishio limeondoka kabisa, na siyo eti tutaacha kuliangazia kabisa,” mkuu huyo wa WHO alisema.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#