Dollar

41,9431

0.01 %

Euro

48,8588

-0.01 %

Gram Gold

5.418,5100

1.69 %

Quarter Gold

9.151,7600

0 %

Silver

65,1400

2.59 %

Viongozi wa upinzani nchini Cameroon wamesema hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa urais, ushindi huo ambao utaendelea kumuweka Rais Paul Biya madarakani kwa kipindi kingine cha miaka saba.

Viongozi wa upinzani Cameroon wapinga matokeo ya uchaguzi

Viongozi hao wanasema matokeo hayo hayaakisi matakwa halisi ya wananchi katika nchi hiyo.

Baraza la Kikatiba la Cameroon siku ya Jumatatu limemtangaza Rais Pual Biya, mwenye umri wa miaka 92, kama mshindi wa uchaguzi, akiwa na zaidi ya asilimia 53 ya kura zote.

Tangazo hilo limechochea maandamano ya ghasia katika miji kadhaa ya taifa hilo. Uamuzi wa mahakama ni wa mwisho na hauwezi kupingwa, jambo linaloweza kuashiria mvutano wa muda mrefu.

Issa Tchiroma Bakary, mpinzani mkuu wa Biya, awali alikuwa ametangaza ushindi wake na kuonya kuwa hatakubali matokeo mengine yoyote.

Wafuasi wake walijitokeza barabarani kwa hasira, wakikabiliana na polisi wa kupambana na ghasia na kufunga barabara katika mji mkuu wa kibiashara, Douala.

Maandamano hayo yalisababisha vifo vya watu wanne mwishoni mwa wiki na wengine wawili Jumatatu, kulingana na vyama vya upinzani.

Hata hivyo, miji ambayo Biya anaungwa mkono ilisherehekea kwa utulivu, huku mitaa ya Douala ikibaki kimya Jumatano kutokana na mvua na uwepo wa polisi wa kupambana na ghasia.

Umoja wa Ulaya ulionyesha “wasiwasi mkubwa” juu ya ukandamizaji wa ghasia za hivi karibuni na kuitaka serikali kutotumia nguvu kupita kiasi. Pia uliwahimiza viongozi kuanzisha mazungumzo ili kuhifadhi utulivu wa taifa.

Viongozi wa upinzani wadai kuibiwa kura

Viongozi wa upinzani wamesema uchaguzi haukakuwa huru na haki, madai ambayo serikali imyakataa.

Akere Muna, wakili maarufu na mgombea wa urais wa zamani, alikosoa mchakato huo kama wa udanganyifu na kuashiria kuwa Baraza la Katiba laegemea upande wa serikali.

Muna, ambaye jina lake lilionekana kwenye karatasi za kupia kura licha ya kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho siku 11 kabla ya uchaguzi na kujiunga na muungano wa upinzani, alisema uchaguzi huo unaonyesha kuendelea kwa mfumo wa miongo kadhaa ulioundwa kudumisha madaraka ya Biya.

“Kilichotokea hakikuwa uchaguzi unaofaa kwa Jamhuri,” alisema Tomaino Ndam Njoya, mgombea pekee wa kike, ambaye alimaliza nafasi ya tano.

“Ilikuwa wizi wa chaguo la wananchi na maslahi yanayopinga uwazi katika mchakato wa kidemokrasia. Napingia matokeo haya,” aliongeza.

Hata hivyo Cabral Libii, aliyeshika nafasi ya tatu, alimpongeza Biya kwa ushindi wake.

Katika mji wa Douala, ambayo wiki iliyopita ilishuhudia baadhi ya maandamano yenye ghasia zaidi, wakazi walijiandaa kuandamana tena Jumanne. Hata hivyo, hali mbaya ya hewa na uwepo wa polisi wenye silaha ulipunguza hamasa ya waandamanaji.

Jean-Pascal, mkazi wa Douala, alielezea ushindi wa Biya kama “ushindi ulioibiwa,” akisema wananchi walipinga serikali ambayo ilifeli kuleta maendeleo kwa zaidi ya miongo minne.

“Wananchi hawakumchagua... Paul Biya. Serikali hii haijaleta chochote kwetu. Kwa miaka 43 – tangu nilipozaliwa – serikali hii imekuwa madarakani. Na haijaleta chochote. Hakuna kabisa,” alisema.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#