Sport
Dollar
41,9729
0.06 %Euro
48,9155
0.07 %Gram Gold
5.345,9700
0.33 %Quarter Gold
9.151,7600
0 %Silver
64,0500
0.87 %Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) limesema Jumanne kuwa wafanyakazi wake watano wa kujitolea wameuawa Sudan.
Wafanyakazi hao watano wameuawa katika jiji la Bara wakiwa wanagawanya chakula na wakiwa wamevaa vazi rasmi la shirika hilo, lisema IFRC, bila kutoa maelezo ya jinsi walivyouwawa au kumtaja yeyote aliyehusika.
Shirika hilo pia limesema wafanyakazi wengine watatu hawajulikani walipo.
Jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) wamekuwa wakipigana tangu Aprili 2023, mapigano ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 20,000 na kuwafurusha watu milioni 14, kulingana na Umoja wa Mataifa na mamlaka za ndani.
Comments
No comments Yet
Comment