Vita imevuruga usambazaji wa mbolea duniani na inaweza kusababisha uhaba wa chakula,

Upungufu wa Mbolea Kutokana na Vita Iran Watishia Usalama wa Chakula.

Vita inayoendelea kuhusisha Iran imeathiri vibaya usambazaji wa mbolea duniani, hali inayozua hofu ya kuongezeka kwa uhaba wa chakula,Kwa mujibu wa wataalamu wa sekta ya kilimo, mbolea ni sehemu muhimu katika uzalishaji wa mazao, na upungufu wake unaweza kupunguza mavuno kwa kiwango kikubwa.

Mkuu wa kampuni ya Yara ameonya kuwa dunia inaweza kupoteza hadi milo bilioni 10 kwa wiki ikiwa hali itaendelea kama ilivyo,Aidha, bei ya mbolea imepanda kwa kasi kutokana na kuvurugika kwa usafırishaji na uzalishaji, jambo linalowaathiri wakulima hasa katika nchi zinazoendelea.

Wataalamu wanasema kuwa hali hiyo inaweza kusababisha ushindani mkubwa wa chakula kati ya mataifa tajiri na maskini, huku maskini wakibaki katika hatari ya njaa.

Chanzo:Newstimeshub 

#