Wachambuzi waibua maswali kuhusu ushawishi wa familia katika taasisi za usalama.
Hatua ya Rais Emmerson Mnangagwa kumpandisha cheo mwanaye Sean Mnangagwa ndani ya jeshi imezua mjadala mkali nchini Zimbabwe kuhusu madai ya upendeleo wa kifamilia katika taasisi za dola.
Wachambuzi wa kisiasa na baadhi ya wananchi wamehoji iwapo uteuzi huo ulifanywa kwa misingi ya sifa za kitaaluma au kutokana na uhusiano wa kifamilia na mkuu wa nchi.
Sean Mnangagwa ni sehemu ya kikosi cha ulinzi wa rais, jambo ambalo limeongeza mjadala kuhusu nafasi ya familia ya rais ndani ya vyombo vya usalama.
Serikali bado haijatoa kauli rasmi kuhusu ukosoaji huo unaoendelea kuongezeka.