Zaidi ya ajira 40,000 zinaweza kupotea kutokana na kusitishwa huko.
Soko kubwa zaidi la nyamba ya ng’ombe kutoka Namibia, Umoja wa Ulaya, limesitisha uagizaji baada ya mlipuko wa ugonjwa wa miguu na midomo, ambao ulisababisha matatizo Ulaya miaka 25 iliopita.
Namibia ilitangaza mwezi uliopita milipuko wake wa kwanza ugonjwa wa miguu na midomo (FMD) kwa mifugo yake katika kipindi cha miaka 60, kusababisha marufuku ya nchi nzima kwa mifugo na uuzaji wa nyama nje ya nchi.
"Umoja wa Ulaya umeamua kusitisha kwa muda kuingiza nyama ya ng’ombe, kondoo na mbuzi ...," Ujumbe wa EU ulitangaza siku ya Jumatatu.
Namibia tayari ilikuwa tayari imetangaza marufuku ya kuuza nyama nje ya nchi mwezi Septemba kabla maamuzi ya sasa hivi ya Umoja wa Ulaya. EU ni soko kubwa la nyama ya ng’ombe kutoka Namibia, ikiwa ni asilimia 80 ya nyama yake ya ng’ombe.
Ajira hatarini
Karibu kilo milioni 10 za nyama kutoka Namibia husafirishwa kwenda Ulaya kila mwaka, balozi wa EU Ana Beatriz Martins alisema katika mahojiano na shirika la habari la Namibia NMH.
Robo ya ajira za moja kwa moja 40,000 zinazohusiana na usafirishaji wa nyama Ulaya zitatatizwa na kusitishwa huko, alisema.
Wakati wa mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa miguu na midomo mwaka 2001, wanyama zaidi ya milioni sita walichinjwa, taarifa ya ujumbe huo ilisema.
Ugonjwa huo umekumba mataifa kadhaa ya kusini mwa Afrika, ikiwemo Botswana, Eswatini, Lesotho, Msumbiji, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe.

