Kanuni hiyo, ambayo ilipitishwa siku ya Alhamisi, itahusisha stesheni za treni zilizopo katika maeneo ya umma, huku katazo hilo, halitohusu hoteli na abiria ambao watapanda na pombe kwenye treni.

Ujerumani yapiga marufuku matumizi ya pombe kwenye vituo vya treni

Shirika la reli la Ujerumani, ‘Deutsche Bahn’, limepiga marufuku matumizi ya vileo katika vituo vya treni.

Shirika hilo, limefikia uamuzi huo, ili kuongeza usalama wa watumiaji wa huduma hiyo, na vile vile kuimarisha usafi wa majiji nchini Ujerumani.

Kanuni hiyo, ambayo ilipitishwa siku ya Alhamisi, itahusisha stesheni za treni zilizopo katika maeneo ya umma, huku katazo hilo, halitohusu hoteli na abiria ambao watapanda na pombe kwenye treni.

Katika utafiti wa hivi karibuni, Deutsche Bahn ilibaini kuwa, asilimia 79 ya wahojiwa, waliunga mkono katazo hilo, huku asilimia 9 pekee, ikipinga marufuku hiyo.

#