Dollar

41,9832

-0.01 %

Euro

48,7827

0.07 %

Gram Gold

5.574,8000

0.13 %

Quarter Gold

9.933,8200

0 %

Silver

66,0800

0.45 %

Tume ya Uchaguzi ya Uganda imetangaza rasmi kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika tarehe 15 Januari. Katika uchaguzi huo, Rais Yoweri Museveni, mwenye umri wa zaidi ya miaka 80, atawania muhula wa saba madarakani.

Uchaguzi mkuu wa Uganda kufanyika Januari 15

Museveni, ambaye sasa ni kiongozi wa nne aliyekuwa kwa muda mrefu zaidi madarakani barani Afrika, serikali yake imebadilisha katiba mara mbili kuondoa kikomo cha umri na muhula wa urais, jambo lililomwezesha kubaki madarakani tangu mwaka 1986.

Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa mwaka 2021, mpinzani wake mkuu anatarajiwa kuwa mwanamuziki maarufu aliyegeukia siasa, Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 43. Bobi Wine ameendelea kuvutia uungwaji mkono mkubwa, hasa kutoka kwa vijana, kutokana na umaarufu wake katika muziki na wito wa mabadiliko.

Maafisa wa chama tawala wanakanusha madai hayo na kusisitiza kuwa Museveni alishinda kwa kupata uungwaji mkono wa kweli kutoka kwa wananchi.

Zaidi ya hayo, wagombea wengine sita kutoka vyama mbalimbali vya siasa pia wamejitokeza kuwania nafasi ya urais.

Uchaguzi huo hautahusisha urais pekee bali pia utajumuisha upigaji kura wa kuwachagua wabunge wa Bunge la Taifa.

Museveni, ambaye ni mwanamapinduzi wa zamani, amesifiwa kwa kuleta utulivu nchini Uganda, kukuza uchumi, na kupambana na ugonjwa wa UKIMWI.

Hata hivyo, wakosoaji wake wanailaumu serikali yake kwa kukandamiza wapinzani wa kisiasa, ukiukwaji wa haki za binadamu, na kashfa za rushwa. Maafisa wa serikali wamekanusha tuhuma hizo na kusema kuwa wanaokamatwa hufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa mujibu wa taratibu za sheria.

Serikali ya Museveni inatarajia kufanya mauzo ya kwanza ya mafuta ghafi nje ya nchi yatakayoanza mwaka ujao kutoka kwenye maeneo yanayoendeshwa na kampuni ya Ufaransa ya TotalEnergies na ile ya China ya CNOOC, yakitarijiwa kusababisha ukuaji wa uchumi kwa kiwango cha juu mara mbili.

Uganda ni nchi muhimu kwa siasa za kijiografia katika Afrika Mashariki na ina wanajeshi waliotumwa Somalia, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Guinea ya Ikweta kama sehemu ya misheni ya kulinda amani, kupambana na waasi au kijeshi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#